Pages

Saturday, April 28, 2018

MAAJABU YA MBOGA ZA MABOGA



 

Mboga za maboga zinatokana na mmea wa maboga. Mboga za maboga huliwa sana na wanyakyusa na wasafwa mkoani Mbeya. Watu wengi wanakula bila kujua faida zake kiafya. Waingereza huita pumpkin leaves.Mboga za maboga zina virutubisho vifuatavyo vitamin A, C, E, B6, calcium, Thiamine, Riboflavin, Niacin, Chuma, Protini, Shaba, Potassium, Magnesium, Phosphorus, manganizi, Nyuzi Lishe na Folic acid.
Mboga za maboga huzuia/ hutibu kifafa kwa kuchanganya majani mateke ya mboga za maboga, maji ya nazi na chumvi kidogo. Na hupewa mgonjwa ale, hupunguza lehemu mwilini, majani ya maboga yana hypoglycaemic kwa wingi yanafaa kuliwa na wanaosumbuliwa na kisukari, Huimarisha afya ya macho, majani ya maboga yana Anti – oxidants kwa wingi yakiliwa hupunguza kuzeeka mapema, majani ya maboga yana nyuzi lishe kwa wingi, vitamin na madini kwa hiyo huzuia uwezekano wa kupata saratani, mboga za maboga huongeza spermatogenesis kwa wingi kwa hiyo hufaa kwa wenye matatizo ya  kutokupata watoto (Infertility), mboga za maboga zina vitamin C kwa wingi hufaa kwa kuimarisha ngozi ya mwili na kutibu vidonda na kuimarisha mifupa, mboga za maboga zinafaa sana kwa mama wanaonyonyesha kwa kuwa zinaongeza kiwango cha maziwa, mboga za maboga huzuia maambukizi ya Bakteria mwilini zikiliwa mara kwa mara, Huongeza kinga ya mwili, Huongeza protini mwilini, mboga za maboga zina nyuzi lishe kwa wingi zikiliwa vizuri na kumfanya mtumiaji kwenda haja vizuri na ni nzuri kwa wenye matatizo ya Anemia.
Pika majani ya mboga za maboga, mafuta ya Alizeti au mzeituni, chumvi kidogo na kitunguu saumu. Pika kwa dakika kumi. Kitunguu saumu weka baada ya kuiva (mwishoni).
Kula mara kwa mara. Wenye kisukari wasiweke chumvi
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya                                                    
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

9 comments:

  1. Asante kwa elimu. Ktk tiba hii ya kifafa hayo majani yanapikwa au yanachanganywa vipi! Na tiba inafanyika kwa mda gani

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa elimu hii nzuri

    ReplyDelete
  3. Wallah mmenikosha kweli kweli

    ReplyDelete
  4. Assente sana kwa kufaidika kwa majani ya maboga

    ReplyDelete
  5. Asante kwa elimu ya lishe

    ReplyDelete