Pages

Saturday, September 20, 2014

MAAJABU YA MCHICHA NAFAKA (GRAIN AMARANTH).



Mchicha nafaka umekuwa ukilimwa na wa Aztecs miaka 8000 iliyopita huko  Mexico na Peru. Siku hizi unalimwa Afrika, India, China, Russia na Amerika ya kusini na Kaskazini. Hapa Tanzania unalimwa kidogo sana labda kwa kutokujua faida zake kiafya.
Mchicha nafaka ni mchicha ambao umefanyiwa utafiti na kuonekana kuwa mbegu zake zinaweza kutumika kama chakula. Mchicha nafaka unaweza kutumika kama mboga za majani na mbegu. Mchicha nafaka ni nafaka  bora katika ulimwengu huu kwa sasa.
Unajulikana kuwa ni nafaka bora ulimwenguni  kwasababu ya virutubisho vingi ulivyonavyo. Mchicha nafaka unavirutubisho vya vitamin, madini, nyuzinyuzi na Amino Acido. Mchicha nafaka ni chanzo kizuri cha Protein,Calcium, Chuma, Magnesium, Potassium, Phosphorus na vitamin A, C na E na Amino acids, lysine kutoka katika kiwango cha  AMINO ACID (Mchicha nafaka una Amino acid 19% na unaweza kutengeneza lysine kiasi cha  5.9-7.1 ukilinganishwa na Maharage ya soya yenye kiwango kikubwa AMINO ACID(3%) lakini yanaweza lysine kiasi cha 2.3 tu (lysine ndiyo inayohusika na kinga mwilini). Mchicha nafaka una protini ya Albumins na Globulins ikilinganishwa na protini iliyomo kwenye ngano itwayo Prolamins ambayo ni ngumu na kusagika. (More soluble and digestible). Mchicha nafaka una vitamin E sawa na mafuta ya Mzeituni (Olive oil). Baadhi ya magonjwa yanazuilika au kutibiwa kwa kutumia mchicha nafaka ni kisukari, Magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease (CVD) Maumivu ya magoti ,maumivu ya vidonda vya koo (mdomoni), Baridi Ya bisi ,minyoo aina ya tegu , kansa ya tumbo ,maziwa ,koo, mapafu nk, kupunguza uzee (Vitamins), Magonjwa ya ngozi ,kuzuia meno kupata kutu ,shinikizo la damu,Huzuia mwili kufa ganzi , Huzuia udhaifu wa misuli , leremu(cholesterol) kwa sababu ya kuwemo ndani ya mchicha nafaka tocotrinols na phytosterols, zinazoondoa lehemu mbaya mwilini. Ugonjwa wa Celiac na matumizi ya mchicha nafaka umethibitika kuwa unaongeza kinga ya mwili (CD4) kwa waathirika wa Ukimwi nk
Pia mchicha nafaka unaweza kutumika kuandaa vyakula mbalimbali kama Uji, Ugali, Chapati, Mikate, Maandazi, Keki, Biskuti, supu, bisi, kuchanganya bisi kwenye wali , mboga za majani (majani ya mchicha) nk.
Watengenezaji wa mikate ya ngano iliyokobolewa ni bora wakaanza kuchanganya mchicha nafaka na ngano wataongeza viini lishe kwenye mikate kwa faida ya afya zetu. Pia mabaki ya mchicha nafaka yanafaa kuandaa vyakula mbalimbali vya mifugo kama ngombe, mbuzi, kuku, nguruwe nk.
Faida zake kwa jamii itaweza kupata viini lishe (Nutrients) tokana na majani au mbegu za mchicha kama protein, starch, madini mbalimbali na vitamin.jamii inaweza kuongeza kipato kwa kuuza mbegu unga nk.
Jamii kwa kutumia mchicha nafaka wataweza kujiongezea kinga na tiba ya maradhi mbalimbali mwilini.
ANGALIZO
Mbegu za mchicha nafaka zina weupe uliofubaa au rangi ya malai(cream).
Kuhusu kupanda na mbegu wasiliana nasi.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


2 comments:

  1. Samaan hivi ili zaoo la mchicha lina soko

    ReplyDelete
  2. Naweza pata mbegu za huo mchicha nafaka

    ReplyDelete