Pages

Thursday, August 31, 2017

KULA MAHINDI YA NJANO UEPUKANE NA KISUKARI




Kwa maoni yangu, mhindi ni mmea wenye utaratibu wa kuvutia. Kuanzia majani yake hadi kwenye mbegu zilizo kwenye hindi lenyewe , kila kitu kimepangwa kwa mpangilio hususa wenye kupendeza.  Isitoshe, mmea huu unapokua “unazungumza” nawe. Unakuambia ikiwa una kiu au hauna lishe ya kutosha.  Kwa kawaida mtoto wa kibinadamu hulia anapohitaji kitu.  Kama tu mimea mingine, mhindi hutoa ishara zinazoonekana, kama vile kubadili rangi na umbo la majani yake, ili kueleza mahitaji yake.  Unahitaji kuelewa ishara hizo.  Huenda majani yenye rangi nyekundu na Zambarau yakaonyesha kwamba mhindi hauna Fosfati.
             Dalili nyingine zinaweza kuonyesha ukosefu wa magnesi, nitrojeni, au potashi. Pia anapoungalia Mkulima anaweza kutambua ikiwa mhindi wake una ugonjwa au umeathiriwa na kemikali.  Mhindi ulianza  kukuzwa huko. Amerika , huenda katika nchi ya Mexico, na kuenea ulimwenguni pote.  Waperu walioishi kabla ya enzi ya wainka waliabudu Mungu wa kike wa mahindi aliyepambwa kwa taji lililotengenezwa kwa bunzi za mhindi. Bunzi hizo zilitokea kichwani mwake kama nyaya katika gurudumu.Wakaaji wa ulaya waligundua mhindi mnamo mwaka 1492 baada ya mvumbuzi Christopher Columbus kuwasili katika visiwa vya karibea.
              Kuna aina nyingi za mahindi zinazogawanya katika vikundi sita vikuu: dent,flint,Flour,sweet,waxy, na popcorn.  Mahindi aina ya sweet hayakuzwi sana kama aina nyingine. Utamu unaopatikana katika aina hii ya mahindi unatokana na kasoro Fulani ambayo huizuia kubadili kiasi cha kutosha cha sukari kuwa wanga.  Zaidi ya asilimia 60 ya mahindi inayouzwa ulimwenguni hutumiwa kulisha mifugo huku asilimia 20  hivi ikilisha  wanadamu.  Asilimia iliyobaki hutumiwa viwandani au kama mbegu. Jina la kibotaniahuitwa ZEA MAYS. Huko India huita CORN (Makai) na Amerika (India corn) haya mahindi ni ya njano mengine ya kawaida na mengine ya Bisi (Popcorn) haya ndiyo nitaelezea umuhimu wake kwa afya zetu.
               Haya mahindi ya njano ya kitumiwa vizuri yanapunguza kuongezeka uzito (weight gain), mahindi haya yana magnesium kwa wingi yanayosaidia kuyaweka matumbo yetu yawe vizuri (wonderful bowel regulator), yanasaidia kujenga mifupa na misuli.  Yana phosphorus kwa wingi inayosaidia kujenga ubongo vizuri na mfumo wa fahamu,Yana madini ya zinki yanayosaidia kuimarisha nguvu za uzazi ukiongeza kikombe kimoja cha unga wa njano kwenye mlo unakua na 2mg za madini ya zinki, kupunguza lehemu kwenye damu (blood cholesterol levels), pia yanamadini ya chuma yanayosaidia kuongeza nguvu mwilini na kinga ya mwili kwa kuzisaidia seli nyeupe za damu ili kupambana na maradhi, yanavitamini “A” nyingi ambayo inatoa kinga dhidi ya magonjwa. Inazuia upofu kwa watoto, inaimarisha misuli ya macho kwa wazee, yana nyuzinyuzi (fiber) ambayo inazuia kisukari na unene,  kuondoa chunusi usoni nk, kuku wa kisasa wakilishwa mahindi ya njano kiini cha yai kinabadilika toka weupe na kuwa njano, hata    kwa upande wa bisi husafisha meno, kuimarisha nguvu za uzazi, kupunguza sukari mwilini, kusafisha damu,hata watu wengine na waathirika wa UKIMWI wazitumie kuboresha afya.Mhindi una kitu kimoja kinaitwa ndevu za mahindi zina faida kubwa kwa binadamu zina Potassium nyingi ambazo zinasaidia kutibu magonjwa yafuatayo kwa wanaokojoa kitandani, maumivu ya tezi dume (prostate), maumivu ya mfumo wa mkojo (UTI) , mawe kwenye figo, moyo kutokufanya kazi yake vizuri(Congestive heart failure), kisukari ukichanganya na Drum stick,uchovu, BP (HBP), kupunguza lehemu (Cholesterd), nk.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



8 comments:

  1. Habari mkuu, nnahitaj mbegu za mahindi ya njano(bisi) ntayapataje? Niko Arusha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari ndugu na Mimi pia nahitaji mbegu ya mahindi ya njano kwa maana ya bisi nipo Rukwa sumbawanga na maelekezo ya sehemu ambayo yanaweza kupandwa joto au baridi

      Delete
  2. Habari Mkuu naomba nijue Mahindi ya njano nayapata wapi ? Hata mbengu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upon maeneo gani naweza kukusaidia kupata mbegu na mahind

      Delete
  3. Inaponya high blood pressure kabisaa??

    ReplyDelete
  4. Article Nzuri sana mkuu. Naweza pata mbegu za mahindi ya njano nipo dar es salaam.

    ReplyDelete
  5. Ujatueleza zaidi hizo ndevu za nahindi unazitumiaje ?

    ReplyDelete
  6. Nashukuru Kwa elimu yako.

    ReplyDelete