Pages

Wednesday, April 6, 2016

MIUJIZA YA MGAGANI KUTIBU MAUMIVU YA HEDHI

Mgagani ni mboga ambayo mwanzo ilikuwa hailimwi ilikuwa inapatikana porini. Siku hizi ni mboga ambayo inapatikana kwenye jumuiya ya watu maskini vijijini. Na asili yake husadikika kuwa Afrika mashariki, Ethiopia, Somalia, Asia kusini na Amerika. Sasa hivi imeenea katika nchi zote za tropiki Afrika, Asia na America.
Na wenyeji wa ukanda wa Kalahari na namib kusini mwa Afrika hutumia majani machanga kama mboga ile ya spinachi. Wahindi na wathai (Thailand) hutumia sana kwa kuwa wanajua faida yake. Jina la kibotania huitwa cleome gynandra. Waingereza wanaita majina African cabbage, spider wisp, cats whisker, spider plants, na bastard mustards.
Wafaransa wanaita caya blanc, br’ede caya na mouzambe. Kwa Kiswahili ni mgagani, mkabili shemsi na mwangani mgange kulingana na maeneo.
Nchini Tanzania ni makabila machache yanayokula mboga hii labda ni kutokana na kutokujua faida zake kwa mwili wa binadamu na wanyama. Mgagani una virutubisho vya kutosha na madini kama vile beta carotene, vitamin C, Chuma, Magnesium, calcium na phosphorus, Protini na amino acid nyingi. Na ni mboga nzuri kwa kuzuia maradhi ya kisukari, Kansa na Magonjwa ya moyo. Pia hutibu maumivu ya kichwa, kufunga choo, maumivu ya tumbo, kuzuia kutapika, diphtheria, vertigo, nimonia (pneumonia), maumivu ya sikio, bawasiri, maumivu ya hedhi kwa wanawake kwa kuchanganya na mimea ya asclepias fruticosa, ulaji wa mara kwa mara kwa wanawake hupunguza uwezekano wa kupata uvimbe wa kizazi, jongo (gout), na anemia. Pia mgagani unafaa kwa akina mama wajawazito wanaotaka kujifungua hurahisisha uzazi na kupunguza maumivu (labor pains ) na kuongeza nguvu mwilini, kutoka maziwa kwa wingi na rheumatism. Mizizi hutibu homa, kuumwa na nge na nyoka. Lakini ni mboga nzuri kwa waliotoka tohara kwani huongeza damu haraka iliyotoka wakati wa kutahiriwa.
Ni mboga nzuri kwa watoto na ili kupunguza uchungu changanya na tui la karanga . Mgagani hupendelea udongo wa mchanganyiko na mchanga usio tuamisha maji. Kwa wakulima unaweza kupanda mgagani na kabeji, collards, French beans n.k ili kuzuia wadudu aina aphid, thrip na diamond back moth. Na wale wanopanda maua aina ya rose kwenye greenhouse wanaweza kupanda ili kupunguza wadudu aina ya red spider mites. Lakini pia unaweza  kutumia majani yake na kuchanganya na maji ya kupulizia shambani ili kupunguza wadudu aina ya aphid na thrip.
Mbegu zake zinaweza kukamuliwa na kutosafishwa mafuta yake hutumika kutengeneza sabuni, bio-fuels na vitu vingine. Majani na mbegu ni chakula kizuri kwa kuku na ndege wengine, ng’ombe, ngamia, farasi na wanyama wa porini wanaofugwa. Tuanze sasa kulima mgagani kwa faida ya afya zetu.
Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil) na Tiba.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya.
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com 

No comments:

Post a Comment