Pages

Wednesday, April 5, 2017

EMBE HUREKEBISHA KIWANGO CHA INSULINI MWILINI


Mwembe hustawi katika maeneo ya joto na nyanda za chini. Mti unafikia urefu wa meta 25, huota maeneo yote ya tropiki. Jina la kibotania huitwa mangifera indica, na waingereza huita mango, wandali na wanyakyusa  huita  umwembe. Maembe  hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tabora, Pwani, Mtwara, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Maembe ni zao muhimu la biashara na chakula. Sehemu zinazotumika ni, Majani Machanga, matunda, kokwa (mbegu), magome (gamba), maua, mizizi nk.  Ili kuyalinda maisha ya mti, chukua magamba kutoka kwenye matawi tu (na iwe kutoka upande mmoja tu)
Tunda hili, licha ya ladha yake nzuri pamoja na utamu wake, linaweza kutumika kwenye milo yote kwa siku kwenye familia nzima.
Ulaji wa mara kwa mara wa tunda hilo husaidia kupunguza kiwango cha asidi mwilini, kuboresha mmeng’enyo wa chakula na kurekebisha kiwango cha insulini. Husaidia kusafisha damu pia, kuimarisha muonekano wa ngozi, kuzuia saratani na kuimarisha kinga ya mwili. Hupunguza mawe kwenye figo. Faida nyingine ni kuongeza madini ya chuma kwa wajawazito, kupunguza uzito na kulinda macho dhidi ya magonjwa.
Unywa wa juisi yake kila siku husaidia kuleta uoni mzuri kwa sababu juisi hiyo ina vitamin A ambayo huimarisha afya ya macho na kuwasaidia wale wenye macho makavu au wasioona vizuri hasa usiku.
Hata hivyo,juisi ya embe inapotumika bila kuweka sukari ni nzuri kwa watu wenye kisukari kwa sababu husaidia kurekebisha tatizo hilo pamoja na kurekebisha mapigo yamoya kuwa sawa na kuondoa sumu mwilini.
Vilevile juisi hii inasifika kwa kuimarisha mmeng’enyo wa chakula na huondoa ukosefu wa choo ikichanganywa na nanasi.
Licha ya vitamin A, juisi ya embe ina vitamin C pamoja na carotenoids ambazo husaidia kurekebisha kinga za mwili hivyo kuwafaa zaidi wenye upungufu wa kinga hizo, wanaonyemelewa na magonjwa au wenye maradhi ya muda mrefu mfano pumu.
Embe linafaida kubwa katika afya ya ngozi kwani ukipaka maganda ya embe usoni na kukaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi kasha ukanawa kwa maji yanayotiririka au yale yanayotoka bombani husaidia kuifanya ionekane vizuri.
Majani machanga ya mwembe yakichemshwa hutibu kuharisha, kuharisha damu, kikohozi, pumu, matatizo ya kifua, homa, bawa siri (haemorrhoids) tumia majani makuukuu na chemsha katika lita 5 za maji kwa dakika 30, chuja na tumia mtokoso huu kwa kuoga sehemu za mapaja, kuoshea kinywa na maumivu ya fizi, kuoshea vidonda vya nje ya mwili, unga wa majani unafaa kwa kutunza meno kwa kusukutulia, maua hutibu minyoo. Tunda lake likiliwa hutibu kuvimba fizi, linaondoa makamasi kifuani kwenye mirija ya hewa, bandama lililotanuka unachanganya na asali kijiko cha chai, matatizo ya tumbo na ini unachanganya na maziwa fresh, vipele vya joto unachemsha maembe 2 mabichi na vikombe 2 vya maji ikipoa unachuja na kuongeza chumvi au sukari kwa ladha, unakunywa mara moja kwa siku, embe bichi vipande 6 vinaweza kuondoa mawe katika figo kwa wiki moja tu vikiliwa kila siku, pigo la moyo ni kuchemsha embe bichi, chumvi na sukari kunywa, ukiinusa sana juisi yake inasitisha utokaji wa damu puani (mhina), na juisi ya embe na maziwa ni kirejesho kizuri cha afya, Tumia mara kwa mara. Unga wa mbegu ukinywa mara 3 kutwa hutibu kuharisha na kuhara damu, uzazi wa majira tumia mbegu ya embe , mbegu ya embe hutumika kulegea kwa uzazi wa mwanamke, na utoaji wa maji meupe kwenye uke, (leucorrhea) . Gome (gamba) hutumika kutoka damu nyingi kuliko kawaida kwa mwanamke, vidonda vya kooni na homa.
Maembe husindikwa ili kupunguza upotevu, kuongeza thamani na matumizi ya zao. Embe husindikwa kupata bidhaa mbalimbali kama vile juisi, achali, chatine na maembe yaliyo kaushwa nk.
Athari, majani makuukuu yatumike kwa kusukutua tu.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com

DENGU HUSAIDIA KUONGEZA NGUVU ZA UZAZI.



Dengu zao muhimu jamii ya mikunde linalolimwa na kutumiwa duniani kote, hasa nchi za kiafrika na kiasia.Jina la kibotania huitwa cicer arietinum l. Waingereza huita chickpea . Ni chanzo kizuri cha wanga na protini, na protini yake inachukuliwa kuwa ni bora kuliko ya mikunde mingine.  Dengu ina kiasi muhimu cha asidi ya amino za msingi kasoro asidi zilizo na salfa “sulphur“ ambazo zinaweza kukamilishwa kwa kuongeza nafaka katika mlo wa kila siku . Kwenye  kuna hifadhi ya wanga , ikifuatiwa na nyuzinyuzi za chakula, oligosaccharides na sukari rahisi kama vile glucose na sucrose. Ingawa kunapatikana kiasi kidogo cha mafuta ( lipids) Dengu ina utajiri wa asidi  za mafuta zisizodhuru muhimu kwa virutubisho kama vile linoleic na oleic acids. Kwenye punje za Dengu pia kunapatikana madini ya calcium , magnesium , phosphorus, chuma na K.
     Dengu ni chanzo kizuri cha vitamin muhimu kama vile riboflavian ( vit B2), niacin ( vit B3), thiamin ( vit B1), Folate na vitamin A (B-Carotene) kama ilivyo mikunde mingine Dengu ina sababu za kuondoa virutubisho visivyofaa ( anti – nutritional factors) kutokana na mbinu mbalimbali za mapishi Dengu zina faida kadhaa kiafya na muunganiko wake   na mikunde na nafaka nyingine unaweza kuwa na athari nzuri kwa magonjwa ya binadamu kama vile kisukari aina ya pili ( type 2 diabetes)  magonjwa  ya mmeng’enyo wa chakula, na baadhi ya saratani, kuondoa udhaifu wa mwili, uchovu na mengineyo, homa, magonjwa ya mfumo wa kupumua na kukojoa, abscesses, husaidia upungufu  wa damu mwilini, hurekebisha lehemu ( cholesterol) na mengineyo.
    Kwa wale wenye kusumbuliwa na matatizo ya nguvu za uzazi  na hawana matatizo ya mzunguko wa damu watumie mara kwa mara, mfumo wa neva , mfumo wa mkojo, homoni na kemikali na utendaji  wa viungo vingine ni vizuri wakatumia Dengu mara kwa mara.  Wananchi wa nchi za Asia kama India , China ,Japan , Indonesia na nyingine zinatumia sana Dengu, soya,  nk. Nchi hizi zina watu wengi duniani kuliko hata  ukubwa  wa  nchi zao.  Na utumiaji wa Dengu mara kwa mara kwa watu wenye kisukari hurekebisha kiwango cha sukari kwenye insulin.  Watanzania wote tuanze kutumia Dengu  mara kwa mara ili kuimarisha nguvu za uzazi kwani sasa hivi  vijana wengi wanalalamika kuwa hawana nguvu za uzazi .
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com

BEETROOT NI NZURI KWA WENYE MAWE KWENYE FIGO


Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya njema kunifikisha 2017. Nilichojifunza ni kwamba watu wengi hawafahamu faida za vyakula tunavyo kula.
Watu wengi hawajui faida za beetroot na hii ndiyo sababu iliyonifanya niandike makala hii ili kuwaelimisha watu wengi. Asili ya Beetroot ni ulaya na imetumiwa na wagiriki na waroma kwa miaka mingi iliyopita. Jina la kibotania Beta vulgaris. Na sasa Beetroot  inalimwa ulimwenguni pote. Kinachotumiwa ni majani na mizizi.
Juisi ya Beetroot ni moja ya juisi bora kwa afya ya binadamu. Beetroot ni chanzo kikuu cha sukari ya asili, calcium, sodium, potassium, phosphorus, sulphur, chloline,iodine,chuma,shaba,choline, vitamin B1,B2, Niacin,B6 na C.
Juisi ya beetroot ni nzuri sana kwa Figo na gall bladder. Madini ya chuma yaliyomo kwenye beetroot yanafaa kurutubisha Anaemia. Juisi ya Beetroot ikichanganywa na karoti na Tango ni nzuri sana kwa wenye upungufu wa nguvu za kiume, mawe ya kwenye Figo,gall bladder, Ini, matatizo ya tezi dume (Prostate troubles) na kutengeneza damu mwilini. Beetroot ni kizuia saratani. Juisi ya beetroot ni nzuri kwa kichefuchefu na kutapika kuna tokana na tindikali (acidity), Homa ya manjano, hepatitis, kuharisha, kutosagika kwa chakula na Dysentery. Juisi hii ichanganywe na juisi ya ndimu ndio inakuwa bora zaidi. Juisi ya Beetroot ikichanganywa na kijiko cha Asali na ikanywewa asubuhi kabla ya kifungua kinywa ni nzuri kwa vidonda vya tumbo aina ya gastric ulcer. Juisi ya majani ya beetroot ikichanganywa na juisi ya ndimu ni nzuri kwa homa ya manjano na vidonda vya tumbo (gastric ulcer)kama inanywewa mara moja kila siku.
Ulaji wa kila siku wa Beetroot huzuia ugonjwa wa kukosa choo na piles.
Juisi ya Beetroot ikitumiwa mara kwa mara utaepukana na magonjwa ya hypertension, arteriosclerosis na matatizo ya moyo.
Wazungu na watu wa Asia hutumia Beetroot kama mboga, salad, juisi na supu.
Watanzania tuanze kutumia Beetroot kwa faida ya afya zetu.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com

MULIMULI HUTIBU TUMBO NA MAGONJWA YA ZINAA






Mulimuli ni mti unaokuwa na kufikia mita 10 hadi 15 kutokana na mazingira uliopo. Hupatikana sehemu nyingi Tanzania. Jina la kibotania hiutwa Cassia abbreviata. Waingereza huitwa Long-pod cassia, longtail cassia, sjambok pod. Kiswahili huitwa Mkakatika au mbaraka.
Wahehe huita Limulimuli, Wagogo huita mkakatika au mulimuli, wasukuma huita Nunda Lunda, wanyamwezi huita Mulunda lunda au munzoka, wasambaa huita mzangazi au msangani, wamwera huita mchenamela, wadigo huita muhumba mkulu, wataita huita msoko.
Mulimuli ni mti unaopendwa sana Africa mashariki kwa matumizi ya dawa kutibu magonjwa mbalimbali. Majani yakivutwa kama sigara hutibu Haematuria, mizizi au unga wa mizizi ikichemshwa na maji hutibu maumivu ya tumbo, kuuma meno unachukuchua, kichocho, matatizo ya gastrointestinal, kisonono, kaswende, Nimonia, matatizo ya uterus kwa wanawake, Hedhi iliyozidi(nzito) kwa wanawake, kuumwa na nyoka, kuongeza hamu ya tendo la ndoa, kuharisha, malaria, Homa, Homa ya Blackwater, minyoo, maumivu ya kifua na vichomi.
Majani yaliyochemshwa na mizizi hufaa kuoshea macho kwa kutibu Ophthalmia. Majani yake yakipondwa hutumika kuwakimbiza nyoka katika mapango yao.
Mulimuli ni rafiki wa mazingira na pia hutumika kutengenezea samani, mitwangio na nguzo za kujengea nyumba n.k.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com

NSEBHE MTI UNAOTIBU MAGONJWA MENGI.


NSEBHE ni mti unaotibu magonjwa.NSEBHE hupatikana katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Morogoro, Tabora, Arusha, Mikoa ya Pwani na Kagera(Rulangaranga) nk. Jina la kibotania huitwa Erythrina Abyssinica. Wanyakyusa huita NSEBHE. Wasafwa huita Lisebhe.
Mti huu sitauelezea sana ila naomba watanzania wote na wale wenye mapenzi mema na mimea, tuupande, tuutunze na kuulinda mti huu kwa sababu hutibu magonjwa mengi sana, Majani hutibu vidonda vya tumbo, kuharisha, vidonda na maumivu ya viungo kwa kuweka kwenye vidonda na kuchua kwenye viungo, kutapisha, kwa wanyama hutibu magonjwa ya ngozi. Maua yakitwangwa hutibu kuhara kwa damu, magome yakirostiwa na kutwangwa kuwa unga yanatibu vidonda vya kuungua, vidonda vinavyotoa usaha na uvimbe. Rojo linalotokana na vishina vya kijani vya mti huu hutibu ugonjwa wa Conjunctivitis unaosababishwa na Chlamydia trachomatis(trachoma).
Magome hutibu Malaria, magonjwa ya zinaa kama kaswende,kisonono, Amiba, kikohozi, kuumwa na nyoka, maumivu ya Ini, maumivu ya tumbo, kusokotwa na tumbo na surua(measles). Maua yakitwangwa hutibu maumivu ya sikio, mizizi hutibu vidonda vya tumbo,malaria, epilepsy, kichocho na blennorrhagia.
Wavuvi hutumia magome yake kama maboya ya kuvulia samaki, pia sisi zamani magome yake tulikuwa tunatumia kutengenezea mihuri kwa matumizi mbalimbali.Mti huu hutumika kutengeneza vinyago, stuli, ngoma, mizinga ya nyuki na bidhaa za mikono. Mbegu zake hutumika kutengeneza urembo wa shanga za kuvaa shingoni.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com