Pages

Sunday, August 24, 2014

MIUJIZA YA BIDENS PILOSA



Licha ya kusambaa kwa mmea huu takribani sehemu nyingi ulimwenguni.Pia uliitwa majina mengi Adenolepis Spp na campylotheca Spp. Wachina  huiita Gui zhen, Wahispania huiita aceitilla au moriseco, USA huiita beggars tick, Spanish needle au needle grass, India huita Ottrancedi, Nchi za kusini mwa afrika huita Uqadoro, Afrika Kusini huita black jack na Brazil huita picao preto au cuamba.
Mmea   huu umesambaa takribani kila kona ya Tanzania na kujipatia umarufu wa kushona nguo (kishona nguo) Wanyakyusa huiita matatila, Wandari huiita Ukapunika , Wameru huiita Manyungunyungu, Wairaqu QALMIR BO. Pamoja na uwezo wake wa ulinzi wa kiafya ukiwemo ule uwezo wa kuongeza na kusafisha damu kwa kasi kuliko hata mchicha, sio jambo la kushangaza. Mtanzania ambaye nyuma ya nyumba yake kuna vishona Kishona nguo akapatikana ana upungufu wa damu.
Majani yake hutumika kamatiba ya maradhi mengi , yakiwemo Malaria, Sickle cell, Kisukari, Macho yenye ukungu Shida ya kukojoa kitandani,Vidonda vibichi Vidonda vya tumbo ,Tumbo kuuma, huangamiza minyoo, Hutibu homa ya vipindi kwa watoto,Gesi tumboni, Colds and flue, Chronic hepatitis, na Mambukizi ya njia ya mkojo (UTI) nk.
Maua yake yakikaushwa na kusagwa kuwa unga huufaa sana kwa kipodozi cha asili kwani huondoa chunusi na kulainisha ngozi.
Mmea huu umekuwa ukiwasaidia sana watu wenye kisukari hasa pale unapochanganya na mchunga (Dandelion) na kula kama mboga mala 1 au mbili kwa siku. Huongeza damu kwa kasi sana ikitumika kama chai ama kama mboga. Pia hutumika kwa watu wenye shinikizo la damu la chini. Kwa kutumia majani mabichi ama yale yaliokaushwa vizuri hasa yaliyo kaukia kivulini yafaa sana kwa chai kuliko majani ya chai ya viwandani ambayo yana aina Fulani ya sumu iitwayo thain.
Husaidia kuondoa sumu mwilini hasa zile zilizo ambatanana na chakula kwa kulisaidia ini, pamoja na Figo ndio maana inapotumika pamoja na mchunga (Tumbaku ya wazuka) huleta manufaa mwilini.
Huondoa tatizo la kufanya choo pamoja na kupunguza uwezekano wakupata saratani ya utumbo mpana na bawasili (Haemorrhoids). Huondoa tatizo la kufunga choo kwa watoto na homa, na malaria kwa matumizi ya maji yaliyochemshwa. Pamoja na mizizi nusu kikombe cha chai kwa muda wa siku tano. Pia huleta hamu ya kula.
Ukichanganya na mchunga (tumbaku ya wazuka)  husaidia sana wanawake wenye hedhi zisizo na mpangilio.Mizizi yake ni bora sana kwa tiba ya malaria na  huweza kuondoo tatizo la kufunga choo.
Mmea mzima hutumika kutibu tonsihitis, Canker sores, kuoshea mdomo na kuongeza maziwa kwa akina mama. Pia ni chakula kwani majani yake machanga yanaweza kuliwa mabichi au yakiwa yameokwa lakini yana radha ya uchungu. Huko Zimbabwe majani yanachemshwa na kuungwa na siagi ya karanga na kuliwa na vyakula vingine. Nchi nyingi za kiafrika zinakula mboga ya majani ya Bidens Pilosa.
Tahadhali.
Usitumie kwa wingi sana inaweza kusababisha kuwasha kwa Figo na bladder.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



MIUJIZA YA AMARANTHUS TRICOLOR




Mchicha wa aina ya amaranthus tricolor L au Amaranthus Gangeticus ni mchicha unaoota sehemu mbalimbali katika nchi yetu. Lakini watu wengi hawautumii labda kwa kutojua faida zake kwa mwili wa binadamu. Mchicha huu ni mwekundu unafanana na mchicha nafaka (grain amaranth). Mchicha huu asili yake ni America kusini (Mexico). Hadi sasa mmea huu umekuwa ukisambaa duniani kote maeneo ya kitropiki na nusu tropiki.
Nchini Indonesia mchicha hulimwa mwaka mzima na hupatikana katika mwinuko wa mita 5 Mpaka 2000 juu ya usawa wa bahari; unalimwa kwenye baridi na joto zaidi unalimwa kwenye rutuba katika maeneo ya chini kwenye eneo la wazi `ambapo hewa na joto ni la kiasi.
Kuna jamii tatu za michicha ambazo ni amaranthus tricolor iitwayo mchicha wa kijani  cha kawaida, Red amaranth ( Blitum rubrum) ambayo shina lake na majani ni mekundu na tatu ni white amaranth (Blitum album) ya kijani nyeupe. Kwenye mchicha huu vinavyotumika ni majani, mizizi na mbegu. Kwenye mchicha huu kuna vitamin A,B,B2,, C, calcium, chuma, magnesium, Phosphorus, Sodium, Potassium, na salfa( sulphur). Pia kuna protini, nyuzinyuzi, wanga na mafuta kidogo. Mchicha huu unatibu magonjwa  kutokuona usiku, mtoto  wa jicho (cataract), bronchitis, asthma, emphysema, kifua kikuu (TB), kufunga choo, kuimarisha fizi, pua, mapafu, kukuza watoto, wakina mama, wajawazito na kuongeza utokaji wamaziwa vizuri, kufunga kuharisha, leucorrhoea, menorrhoagia, uhanithi, kutibu sehemu zenye maumivu na mbegu zake huimarisha nguvu uzazi na uhanithi (impotence).
Watanzania tuanze kutumia mchicha huu kwa faida ya afya zetu.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



MAAJABU YA WITHANIA SOMNIFERA. Wasukuma wanauita MTEMUA SHIMBA




Withania somnifera (winter cherry) unastawi kwa mtindo wa vichaka na kukua hadi kufikia kimo cha mita 1.5 (moja na nusu ). Huzaa matunda ambayo yakikomaa huwa mekundu na mbegu zake huwa za njano. Mmea huu una alkaloid somniferine. Mizizi yake ina mafuta ( essential oil) pia ina madini ya potassium nitrate na glucose .
Mmea huu katika Tanzania hupatikana katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Njombe, Iringa, Morogoro, Tanga, Tabora, Singida, Mwanza, Kagera, Shinyanga,   Dodoma , Kilimanjaro  na Arusha. Mmea huu hutibu magonjwa mbalimbali kama ugumba kwa wanawake,  matatizo ya udhaifu wa mwili, rheumatism, kifua kikuu ukichanganya na pilipili manga na asali,  kukosa usingizi, kikohozi na baridi,  matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji chakula,  kukosa hamu ya kula chakula,  kuumwa vidonda vya tumbo (gastric ulcer) , hurahisisha utokaji wa mkojo vizuri,  hutibu baadhi  ya magonjwa ya ngozi, majipu, kuvimba mikono na miguu, kuua chawa mwilini , matatizo ya macho (sore eyes ) kuimarisha nguvu za uzazi (hasa kwa wale wanaowahi  tendo la ndoa) na kutibu maumivu baada ya kujifungua.
Matunda yake yanapendwa sana na baadhi ya ndege  na watu wengine hupanda kama  maua majumbani mwao .
TAHADHARI.
Wajawazito wasitumie inaweza kuharibu mimba .
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com





MAAJABU YA PARACHICHI (AVOCADO-PERSEA AMERICANA MILL)



Wanyakyusa  na wandali  huita takapela au kasokela. Ni mti  wenye urefu  wa hadi meta 20. Asili yake ni  amerika  ya  kusini  katika  nchi  ya Mexico  na  nyingine. Wenyeji wa Mexico  wa Aztec  neno Avocado lenyewe linatokanana na  neno la Nahuatl  ‘ahuacatl’ ni kifupi  cha neno la kia-Aztec ‘ahuacacuahatl’ likimaanisha mti wa kende/korodani (testicle tree). Parachichi lilipelekwa Ulaya na wahispania  walioenda Amerika ya kusini miaka mingi iliyopita. Hapa Tanzania parachichi  lililetwa na wajerumani na  waingereza kwa nyakati tofauti. Hapa nchini ni watu wachache wanaojua faida za mti huu. Tunashukuru kwa hapa Tanzania, Chuo kikuu cha Sokoine, Tengeru na taasisi  ya  utafiti ya kilimo  Uyole  Mbeya zinafundisha  na kuzalisha parachichi zinazokua kwa muda  mfupi kuanzia miaka miwili na nusu na kuendelea kwa njia ya kupandikiza ‘grafting’. Parachichi (Avocado) ni mojawapo ya matunda ambayo yanatunza na kukuza mwili. Yana vitamini nyingi sana, madini na pia mafuta halisi yanayopatikana kwenye vyakula,  yaani yasiyotengenezwa na binadamu parachichi ina madini, nyuzi na vitamini. Parachichi lina ubora wa vitamin C, B6 na E ambazo ni vitamini muhimu sana za kukuza mwili na pia kwa  afya ya ngozi. Vitamini B6, ukosefu wa vitamin hii huleta kufadhaika  yaani  “mood swings”. B6 pia husaidia  kupunguza maumivu yanayoletwa na hedhi  yaani ‘Premenstrual stress’ PMS. Vitamin C ni muhimu  kwa kuponya vidonda vya ngozi pia husaidia mwili kujikinga na magonjwa  kama mafua na ugonjwa  wa  kuvimba ufizi unaotoa damu  yaani ‘scurvy’. Parachichi ni bora kwa watu  walio  katika  hali  ya kupona  baada  yakuugua  na wale wanaougua pia. Vitamini E  hupunguza kuchoka kwa  akili na  kuongeza  tukio la  uzazi (Upungufu  wa nguvu za  kiume). Vitamini  hii pia ni muhimu kwa afya  ya  ngozi. Madini K+ ni muhimu sana  kwa  maisha ya chembechembe  za mwili  ‘Cells’. K+ ni muhimu kwa  afya kwa sababu  upungufu wake huleta ugonjwa wa kujisikia mlegevu  au kupungukiwa na nguvu. Madini ya parachichi  ni muhimu kwa kukuza mtoto aliye bado tumboni  mwamaake. Parachichi pia matukio ya saratani  furani haswa zile za mdomo  na kishimo kilicho nyuma ya pua, kinywa na koromeo (yaani pharynx) na pia ugonjwa wa moyo. Parachichi ina manufaa kwa mzuguko wa damu mwilini. Majani machanga ni dawa ya kikohozi, yakitokoswa kwenye maji  na yaliyokauswa  kijani nyeusi  ni dawa ya kuharisha. Majani huongeza  damu mwilini [anemia], kuumwa kichwa, koo, tumbo, uchovu, kuimarisha meno na kuondoa maumivu. Maganda [barks] yanafaa kwa kutengeneza dawa rheumatism kwa kuchanganya na mafuta ya mboga mboga. Peke la parachichi ni rafiki mkubwa wa moyo  wa binadamu, majipu, kuimarisha kinga ya mwili na shida ya mkojo  kukwama. Parachichi  hutumiwa  vizuri hufanya kazi ya kuokoa nywele  zinazoanguka (upaa) kama litapakwa pale na husaidia kukuza nywele  zinazodumaa (dandruff). Pia hutumika kwenye vipodozi  mbalimbali. Parachichi hutumika kwa kutengenezea  kinywaji cha parachichi. Kupaka kwenye mkate, ndizi, viazi, magimbi, kutengeneza kachumbali ,guacamole, avocado na saradi ya nyanya, na avocado spread.
Tunapenda kila famiilia kutumia parachichi katika mlo ili kuboresha afya zetu.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com





MAAJABU YA CHOROKO ( CICER ARIETINUM L )




Choroko zao muhimu jamii ya mikunde linalolimwa na kutumiwa duniani kote, hasa nchi za kiafrika na kiasia. Waingereza huita chickpea . Ni chanzo kizuri cha wanga na protini, na protini yake inachukuliwa kuwa ni bora kuliko ya mikunde mingine.  Choroko ina kiasi muhimu cha asidi ya amino za msingi kasoro asidi zilizo na salfa “sulphur“ ambazo zinaweza kukamilishwa kwa kuongeza nafaka katika mlo wa kila siku . Kwenye  kuna hifadhi ya wanga , ikifuatiwa na nyuzinyuzi za chakula, oligosaccharides na sukari rahisi kama vile glucose na sucrose. Ingawa kunapatikana kiasi kidogo cha mafuta ( lipids) choroko ina utajiri wa asidi  za mafuta zisizodhuru muhimu kwa virutubisho kama vile linoleic na oleic acids. Kwenye punje za choroko pia kunapatikana madini ya calcium , magnesium , phosphorus, chuma na K.
            Choroko ni chanzo kizuri cha vitamin muhimu kama vile riboflavian ( vit B2), niacin ( vit B3), thiamin ( vit B1), Folate na vitamin A (B-Carotene) kama ilivyo mikunde mingine choroko ina sababu za kuondoa virutubisho visivyofaa ( ant – nutritional factors) kutokana na mbinu mbalimbali za mapishi choroko zina faida kadhaa kiafya na muunganiko wake   na mikunde na nafaka nyingine unaweza kuwa na athari nzuri kwa magonjwa ya binadamu kama vile kisukari aina ya pili ( type 2 diabetes)  magonjwa  ya mmeng’enyo wa chakula, na baadhi ya saratani, kuondoa udhaifu wa mwili, uchovu na mengineyo, homa, magonjwa ya mfumo wa kupumua na kukojoa, abscesses, husaidia upungufu  wa damu mwilini, hurekebisha lehemu ( cholesterol) na mengineyo.
            Kwa wale wenye kusumbuliwa na matatizo ya nguvu za uzazi  na hawana matatizo ya mzunguko wa damu, mfumo wa neva  mfumo wa mkojo, homoni na kemikali na utendaji  wa viungo vingine ni vizuri wakatumia choroko mara kwa mara.  Wananchi wa nchi za Asia kama India , China ,Japan , Indonesia na nyingine zinatumia sana choroko, soya, dengu nk. Nchi hizi zina watu wengi duniani kuliko hata  ukubwa  wa  nchi zao.  Na utumiaji wa choroko mara kwa mara kwa watu wenye kisukari hurekebisha kiwango cha sukari kwenye insulin.  Watanzania wote tuanze kutumia choroko  mara kwa mara ili kuimarisha nguvu za uzazi kwani sasa hivi  vijana wengi wanalalamika kuwa hawana nguvu za uzazi .
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



FAIDA ZA TENDE KATIKA MWILI




Katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, tende ndio tunda linaloliwa kwa wingi,pengine kuliko tunda linguine. Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia lime thibitika kusheheni madini na vitamin lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya. Katika makala hii, nimekuorodheshea faida 10 za tende:
1.      Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hilo.
2.       Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1,B2, B3,B5, A1na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili kwa ujumla.
3.      Ulaji wa tende huimalisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinacho sababisha maumivi wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.
4.      Ukila tende, mwili utapata nguvu na kuondolea uchofu ndani ya nusu saa, kwasababu tende ina virutubisho vya asili kama vile ‘glukosi’ ‘sucrose’na fructose’. Ili kupata faida za tende, changanya na maziwa fresh kasha kula. Pindi unajisikia mchofu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ina shauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kurejesha mwili wako nguvu, iliyopotea siku nzima.
5.      Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishwaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji wa vyakula vinavyotengeneza ‘potassium’ huweza kumwepusha mtu kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza cholesterol mwilini na LDL Cholesterol.
6.      Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), waweza kupata haueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango chakutosha cha madini ya chuma ambayo huitajika utengenezaji wadamu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
7.      Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kasha asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini.
8.      Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalumu wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.
Asubuhi, sisage tende kwenye maziwa hayo hadi zichanganyike, kasha weka asali kiasi cha vijiko vitatu ua vine  vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo, Kisha kunywa mchanganyiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.
          9 Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina mana kwamba, wale wanahitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.
10   Tende inatibu saratani ya tumbo. Hata hivyo tende ni tiba kama tiba nyingine na haina madhara  yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kuona usiku (night blindness).
     Kwa ujumla faida za tende ni nyingi na unaweza kuila  tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizo 10 na nyingine.

MAAJABU YA CENTELLA ASIATICA KUIMARISHA KUMBUKUMBU (IMPROVING MEMORY)





CENTELLA ASIATICA au Gotu Kola, Indian Pennywort, Marsh Penny ni mmea unaoota kwa kutambaa. Na huota sehemu zilizo na unyevu mwingi na kwenye kingo za mito. Mmea huu umekuwa ukitumika sana huko mashariki ya mbali India, China, Japan, Indonesia na nchi za Amerika. Hapa nchini Tanzania ni watu wachache sana wanaotumia, na hii inatokana na watu wengi kutoufahamu kazi yake japo wanauona wanapokuwa kwenye shughuli zao nyingine. Mmea huu una virutubisho vingi vinavyoweza kumsaidia binadamu kuboresha afya yake. Watu wengi wakifikia umri wa miaka 50 na kuendelea kumbukumbu zao kichwani huanza kupungua. Mmea huu ukitumiwa vizuri utaimarisha kumbukumbu zetu vizuri. Mmea huu hauishii hapo tu unatibu na magonjwa mengine kama kisukari huko India, China, Japan, Indonesia n.k hutumia sana. Magonjwa ya kuharisha damu kwa watoto katika hatua za mwanzo na matatizo ya tumbo kwa watoto. Matatizo ya tumbo kwa watoto huchanganywa na majani ya Fenugreek (Methi kwa kihindi). Ni mmea mzuri kwa mfumo wa neva (Nervous Disorders). Ni mmea mzuri kwa watu wenye matende (elephantiasis) juisi yake hupakwa sehemu zilizoathirika.
Pia ni mmea mzuri sana ukichanganywa  na mmea wa Trichodesma Indicum kutibu utasa kwa wanawake (Female Sterility) Hapa ni vizuri tukaelewana kuwa mwanamke asiwe na matatizo ya hedhi (Menstrual Pain) kutoka uchafu sehemu za siri (Usaha), uzito mkubwa sana n.k kama ana matatizo haya atibu kwanza. Pia hutibu magonjwa ya ngozi na vidonda vinavyotokana na kaswende. (Syphilitic Sores).
Pia majani yake huko India hutumika kutengeneza supu, Chatne, Chai, Juisi na kuchanganya kwenye chapati. 

Tahadhari: Inashauriwa kutumia juisi kidogo ya mmea huu kwa sababu ina nguvu sana.
Kwa kuwa huu mmea unaweza kupanda kwenye bustani au kwenye makopo ya kupandia maua tunashauri kila familia ipande ili kuboresha afya.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si ahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


DANDELION (Taraxacum Officinale) Mmea unaofaa kwa kuimarisha mifupa ya mwili





Dandelion ni mmea jamii ya mchunga. Ni mmea wenye faida nyingi kwa binadamu. Mmea huu asili yake ni ulaya na huko mashariki ya mbali India. Na hapa Tanzania hupatikana porini na majumbani kama maua. Na wenyeji wa Tanga, Pemba, Unguja na Mombasa (Kenya) huiita kwa jina la tumbaku ya wazuka. Dandelioni ina chumvi nyingi ambayo ina faida kwa kiwiliwili (mwili) cha binadamu na vilevile ina vitamin A, B, C ina protin, mafuta, wanga, chuma, calciaum, phosphorus, Magnesium, sodium, potassium, Thiamine, (B1), Riboflavin (B2) kuwemo kwa madini mengi ya asili ya magnesium ndiko kunakofanya mmea huu kuwa muhimu katika kuimarisha mifupa. Kinywaji cha juisi ya majani au miziz kinafaa sana kwa matatizo mifupa. Na juisi yake ikichanganywa na juisi ya karoti ndiyo inafaa sana. Ni dawa nzuri sana kwa ini kwani husaidia ini kufanya kazi yake vizuri na kutoa sumu zanye madhara. Dandelion (Tumbaku ya Wazuka) hutumika kama dawa ya Romatizim (Rheumatism) kukosa damu (Anemia), matatizo ya mkojo, chunjua (warts), matatizo mengi ya mwili figo, kisukari n.k
Pia dandelion hutumika kwenye saladi, supu na chai kwa ajili ya kuboresha afya zetu. Tunashauri kila familia ipande nyumbani kama wanavyopanda maua.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Matatizo ya meno, Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com