Pages

Saturday, May 11, 2013

Mapishi mbalimbali

WALI WA MCHELE NA TUI LA KARANGA

MAHITAJI  : Mchele
                     : Tui la Karanga
                    : Chumvi
                     : Maji

Utayarishaji na mapishi
Ø  Chagua Mchele
Ø  Loweka unga wa Karanga kwa maji safi ya vuguvugu kwa dakika 10
Ø  Kamua tui kwa kutumia maji ya vuguvugu hii inasaidia kutoa tui na lenye mafuta mengi
Ø  Weki tui jikoni linapokaribia kuchemka punguza tui zito la juu na hifadhi vizuri.
Ø  Ongeza mchele, koroga, usifunike. Pika hadi maji yabakie kidogo, halafu funika
Ø  Ongeza tui ulilopunguza (tui zito). Punguza moto kabisa ivisha taratibu ukishakaukia geuza
Ø  Palia kwa dakika 10-15 wali utakuwa tayari

MATUMUZI:-
Kula pamoja na nyama au samaki au maharage na mboga za majani na matunda
¬  Machicha ya karanga yanayoaaaabakia yanaweza kutumika kuungia mboga ya majani au maharage.*

Imeandaliwa na Edgar Kajolo Kapagi           Mbeya
MOBILE: 0754 807401 – 0788 029500

2: UJI WA KIMEA
MAHITAJI:-  Unga wa nafaka ya mahindi au mtama au ulezi iliyooteshwa, kukaushwa
                      na kusagwa.
                   :  Sukari
                   :  Maji
                   :  Chumvi

Utayarishaji na mapishi.
  • Pima unga wa kawaida wa mahindi au mtama
  • Pika uji mzito mpaka uive kabisa
  • Epua, pooza kidogo
  • Ongeza unga wa kimea kiasi cha kijiko kimoja au zaidi kulingana na kiasi cha uji uliopika, endelea kukoroga mpaka uji ulainike.
  • Rudisha tena uji jikonoi chemsha kwa muda  ongeza sukari au chumvi
  • Epua

Matumizi.
Mlishe mtoto kwa kutumia kijiko na kikombe au sahani au bakuli. Pia unaweza kutumika kama kifungua kinywa kwa watoto wa shule na Familia.

Kumbuka : unaweza kuongeza karanga au maharage au mboga za majani au unga wa Soya au yai au maziwa  kuongeza ubora wa uji unga wa kimea unasaidia kulainisha uji wa mtoto na kumfanya anywe kiasi kikubwa kumwezesha kupata viini lishe vya nguvu kwa wingi.

Imeandaliwa na Edgar Kajolo Kapagi            Mbeya
MOBILE: 0754 807401 – 0788 029500

No comments:

Post a Comment