Pages

Saturday, September 20, 2014

MAAJABU YA MAFENESI ( ARTOCARPUS HETEROPHYLLUS LAM)




MAFENESI au Jackfruits kwa lugha ya kiingereza na majina mengine Langka na Nangka ni matamu kwa ladha yake. Lakini pia yana umuhimu katika mwili wa binadamu.
Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats).
Lakini kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na Tanzania,
Na nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Mbeya(Kyela) nk.
Na sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.
Mafenesi yana vitamin B1 na B2, vitamin C, flavonoids na ni chanzo kizuri cha carotenoids na Potassium nk. Katika nchi kama Thailand majani machanga na maua machanga ya kiume hupikwa kama mboga. Matunda yaliyoiva hulimwa yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa na nazi au hutengeneza ice cream, chatine(chutney), jam, jeli, (jelly) na pesti.
Mfenesi una faida nyingi tukianzia na majani hutibu homa  magonjwa ya ngozi majipu, vidonda na kisukari. Tunda lina wingi wa vitamin C ambayo kiafya inasaidia kuongeza kinga ya mwili, tunda hili linasaidia kupunguza mafua, kifua na homa. Vitamin C hiyo husaidia kuondoa sumu mwilini na kuukinga mwili na maradhi pale linapotumiwa ipasavyo.
Fenesi pia linasaidia kuupa mwili nguvu kwani lina madini ya wanga na sukari ambayo husaidia kuupa mwili nguvu kwa haraka. Fenesi linaweza kuondoa sumu mwilini hivyo linakinga na saratani za aina mbalimbali kama ile ya mapafu. Mdomo na kinywa  na tumbo. Fenesi hutia nguvu mwili na kwenda haja vizuri. Kwa wale wenye matatizo ya shinikizo la damu, Fenesi ni tiba nzuri kwani ina madini ya potassium ambayo husaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza uwezekano wa kupata  shinikizo la damu na kukuondoa katika hatari ya kupata kiharusi. Mizizi yake hutibu homa, kuharisha, magonjwa ya ngozi  na asthma. Utomvu wake ukichanganywa na siki hutibu tambazi (abscesses), kuumwa na nyoka na uvimbe wa tezi (glandular) nk. Magamba yake hutibu vidonda kwa kuweka kibandiko (poultices)
Mbegu zake zikikaangwa huongeza tendo la kujamiiana.
Watanzania tuanze kula fenesi baada ya kula husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula kwa sababu ni tunda muhimu na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa. Pia kwa wenye matatizo ya macho na kutokuona vyema, tunda hili ni mkombozi mkubwa  kwani lina wingi wa vitamin C ambayo huongeza kiwango cha kuona (uoni), pia lina uwezo wa kuondoa sumu, hufanya kazi katika retina na kuifanya iwe imara.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

6 comments:

  1. Asante Sana kwa elimu Na kutufariji kwa namna moja ama nyingine Asante Sana

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa elimu hiyo ya kilimo cha mafenesi. Binafsi napenda kujua wapi nitapata mbegu za mafenesi yenye kuzalisha matunda bora.

    ReplyDelete
  3. Asante sana kwa elimu hiyo ya kilimo cha mafenesi. Binafsi napenda kujua wapi nitapata mbegu za mafenesi yenye kuzalisha matunda bora.

    ReplyDelete
  4. Hakika watu huangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6) Mungu ameumba kila aina ya tunda kama dawa ila wanadamu kwa kupuuza tunapatwa na magonjwa. Asanteni kwa uchanganuzi went. Barikiwa na BWANA.

    ReplyDelete
  5. Hakika watu huangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6).

    ReplyDelete
  6. Shukrani nlikua nauliza inaweza kutibu athritis

    ReplyDelete