Pages

Friday, September 6, 2013

MAAJABU YA MTI HUU-DRACAENA USAMBARENSIS



 
DRACAENA USAMBARENSIS
(Tetesyeri, Tsheleli-Kisafwa, Msigandi, Mukwanga-Wadigo, Mtetemu-Wamwera)
Dracaena, Usambarensis au Tetesyeri, Tsheleli-kisafwa ni mti unaopatikana katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Ruvuma na Tanga(Lushoto) nk.
            Mti huu umeonekana kuwa na faida kubwa sana kwa afya ya binadamu kwa vile hutibu maradhi mbalimbali. Mti huu umekuwa ukitumiwa na mababu zetu toka siku  nyingi. Mti huu hutumika hata kwenye matambiko mbalimbali kwa mfano kukiwa na uhaba wa mvua wazee wa kisafwa hutumia kutambikia na uhaba wa mvua unatoweka na hata kama yatatokea maradhi ya ajabu ajabu. Pia miti yake hupandwa kuzunguka zizi la ng’ombe kuzuia watu wabaya(wachawi) ili wasiharibu mifugo na watu wengine hupanda majumbani mwao kama maua. Pia watu wengine  hutumia majani yake kumuoshea mtu anayesadikiwa amerogwa. Majani yake hutumika kutoa kondo la nyuma kwa mwanamke aliyetoka kujifungua. Pia majani yake ni dawa ya degedege kwa watoto. Mizizi yake hutibu maumivu ya tumbo hasa linaloandamana na kisonono. Pia mizizi hutumika kwa maumivu ya kifua . Hili ni muhimu kwa kila Mtanzania kulifanyia utafiti zaidi kwani watu wengi wamepanda hasa wenye nyumba za kisasa hata baadhi ya makanisa hutumia kupamba wakati wa sherehe mbali mbali kama maua.  Pia mti huu unatunza mazingira kwenye vyanzo vya maji. Napenda watanzania wenzangu waujue huu mti manufaa yake kwa jamii.
                        Dr Edgar Kajolo Kapagi.
Mazingira Natural Product Mbeya
Simu namba: 0754807401

No comments:

Post a Comment