Pages

Wednesday, November 6, 2013

MAAJABU YA Gotu Kola



KUIMARISHA KUMBUKUMBU (IMPROVING MEMORY)
CENTELLA ASIATICA au Gotu Kola, Indian Pennywort, Marsh Penny ni mmea unaoota kwa kutambaa. Na huota sehemu zilizo na unyevu mwingi na kwenye kingo za mito. Mmea huu umekuwa ukitumika sana huko mashariki ya mbali India, China, Japan, Indonesia na nchi za Amerika. Hapa nchini Tanzania ni watu wachache sana wanaotumia, na hii inatokana na watu wengi kutoufahamu kazi yake japo wanauona wanapokuwa kwenye shughuli zao nyingine. Mmea huu una virutubisho vingi vinavyoweza kumsaidia binadamu kuboresha afya yake. Watu wengi wakifikia umri wa miaka 50 na kuendelea kumbukumbu zao kichwani huanza kupungua. Mmea huu ukitumiwa vizuri utaimarisha kumbukumbu zetu vizuri. Mmea huu hauishii hapo tu unatibu na magonjwa mengine kama kisukari huko India, China, Japan, Indonesia n.k hutumia sana. Magonjwa ya kuharisha damu kwa watoto katika hatua za mwanzo na matatizo ya tumbo kwa watoto. Matatizo ya tumbo kwa watoto huchanganywa na majani ya Fenugreek (Methi kwa kihindi). Ni mmea mzuri kwa mfumo wa neva (Nervous Disorders). Ni mmea mzuri kwa watu wenye matende (elephantiasis) juisi yake hupakwa sehemu zilizoathirika.
Pia ni mmea mzuri sana ukichanganywa  na mmea wa Trichodesma Indicum kutibu utasa kwa wanawake (Female Sterility) Hapa ni vizuri tukaelewana kuwa mwanamke asiwe na matatizo ya hedhi (Menstrual Pain) kutoka uchafu sehemu za siri (Usaha), uzito mkubwa sana n.k kama ana matatizo haya atibu kwanza. Pia hutibu magonjwa ya ngozi na vidonda vinavyotokana na kaswende. (Syphilitic Sores).
Pia majani yake huko India hutumika kutengeneza supu, Chatne, Chai, Juisi na kuchanganya kwenye chapati.
Tahadhari: Inashauriwa kutumia juisi kidogo ya mmea huu kwa sababu ina nguvu sana.
Kwa kuwa huu mmea unaweza kupanda kwenye bustani au kwenye makopo ya kupandia maua tunashauri kila familia ipande ili kuboresha afya.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si ahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

No comments:

Post a Comment