Pages

Monday, September 5, 2022

MAJI: SEHEMU MUHIMU YA MLO WA BINADAMU

 

Kwanini tunahitaji maji mwilini.?

Je tunahitaji maji kiasi gani.?

Haya ni maswali ambayo kila binadamu anapaswa kujiuliza, kwasababu haina maana yeyote kama tunakunywa maji kila wakati,lakini tusijue faida yake mwilini.

Maji ni muhimu kwa makuzi na ulinzi wa miili yetu kwa kuwa yana kazi nyingi za mchakato wa kibaolojia mwilini.

Maji ni sehemu muhimu ya mlo wowote wa binadamu na hata  wanyama.Ndio maana mtu yeyote akishakula lazima atatafuta  maji ya kunywa. Katika mwili wa mtu mzima, asilimia kati ya 50 hadi 70 ya uzito wake ni majimaji, na bila maji muda wa uhai wa mwili unakuwa hatarini katika kipindi cha saa au siku chache.

Watu wengi hawanywi maji ya kutosha kwa siku, na matokeo yake ni kukaukiwa maji mwilini, na kusababisha madhara mengine kama ya kuumwa kichwa, uchovu na kushindwa kuwa makini.Mchakato wote wa lishe hauwezi kufantika vizuri bila ya maji. Maji ni muhimu sana mwilini kwani: Hurekebisha joto la mwili, Husaidia katika uyeyushaji wa chakula

Kukauka maji kwa muda mrefu mwilini kunaweza kuchangia matatizo kadhaa ya kiafya kama vile kutoenda haja kubwa na ugonjwa wa figo.

Je unahitaji maji kiasi gani.?

Kwanza ni muhimu kuanza kunywa maji angalau glasi moja tu mara unapoamka  asubuhi.

Pili jiwekee birika la maji mezani kwako, iwapo upo kazini, ili iwe rahisi kwako kunywa maji kila unapohitaji wakati wa kazi.

Kama upo katika mahangaiko wakati wote wa mchana, ni vyema ukabeba chupa ya maji, ili uweze kunywa maji wakati wote utakapojisikia kiu.

Ongeza kiwango chako cha ulaji matunda na mboga, kwani mboga na matunda yana kiwango kikubwa cha maji na faida nyingine kadhaa za kiafya.

Mwili wa binadamu na wanyama hupata maji yake kwa njia kuu tatu. Kwanza kunywa maji yenyewe kama kinywaji au kwakunywa viburudisho vingine kama vile soda. Maji pia yapo katika vyakula vigumu tunavyokula.

Yapo pia maji yanayotengenezwa katika mwili ikiwa ni matokeo ya mmeng’enyo wa kikemikali ndani ya mwili.

Mtu mzima kwa wastani anatakiwa kunywa angalau lita 2.5 za maji kwa siku, kati ya kiasi hiki, 1.8 lazima ipatikane kwenye vinywaji halisi, ikiwa na maana ya glasi 6 au 7 hivi kwa siku.

Unywaji huu unatakiwa kuongezwa wakati wa majira ya joto au baada ya kufanya kazi iliohitaji nguvu ili kurejesha uwiano wa maji katika mwili.kunywa maji yasiyochanganywa na chochote,bado ndio njia madhubuti ya kurejesha maji yanayopotea kutoka mwilini.

Maji ni mojawapo ya zawadi ya pekee ambayo mungu alitupatia. Karibia magonjwa yote yanayomsibu mwanadamu yanatibika kwa kuyatumia maji tu. Unapotumia Tiba ya maji unaepukana na kuumwa ugonjwa wa kichwa, presha, upungufu wa damu, kupooza, mapigo ya kasi ya moyo na kuzimia,kikohozi,pumu,kifua kikuu,kiungulia,kuharisha damu, bawasiri,kisukari,,matatizo ya macho,matatizo ya pua,masikio na koo.

Baada ya kuamka asubuhi mapema, kabla ya kupiga mswaki na kunawa uso, kunywa bilauri nne za maji, usile wala kunywa chochote mpaka dakika 45. Baada ya kunywa bilauri za maji ndipo upige mswaki na kunawa uso. Usinywe maji pale umalizapo kula chakula cha asubuhi, cha mchana  au cha usiku hadi baada ya saa moja au saa mbili zipite epuka kwenda kulala mara tu baada ya kumaliza kula chakula.

Kwa wagonjwa waliodhaifu inashauriwa waanze mpango huu kwa wakunywa bilauri moja au mbili na polepole waongeze idadi hata kufikia bilauri nne. Shinikizo la damu kunywa mwezi mmoja, matatizo ya gesi siku kumi, kufunga choo miezi sita, kisukari mwezi mmoja, kifua kikuu miezi mitatu, saratani miezi sita, Tumia maji salama kila wakati.

 

No comments:

Post a Comment