Pages

Wednesday, April 23, 2014

KITUNGUU SAUMU ( ALLIUM SATIVUM) KIUNGO RAFIKI MKUBWA WA MOYO WA BINADAMU.




Kitunguu saumu asili yake ni asia ya kati na kimekuwa kikilimwa kwa karne nyingi katika nchi za mediteranian na uingereza kuanzia karne ya nne ya 16. Nchini china kilijulikana miaka 3000 iliyopita kabla ya Kristo. Leo hii nchini China kitunguu saumu kinatumika katika  mapishi mbalimbali na kutibu magonjwa mbalimbali. Kwa sasa kitunguu saumu kinalimwa India, Philippine, Brazil,Mexico, na baadhi ya nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania.
Kitunguu saumu kina manufaa makubwa katika mwili wa binadamu, kiasi kwamba ni rafiki mkubwa wa moyo,mbali na kuusaidia moyo usikumbwe na maradhi, kitunguu saumu pia kinazuia saratani , huingizwa oksijeni inapotakiwa , hupunguza shinikizo la damu na kolestrol, hupambana na septini, bacteria, kuganda damu na ute. Kiungo hicho cha chakula huhami mwili  dhidi ya utitiri wa vimelea na bacteria, fangasi na maambukizi ya virusi vingine. Pia huimarisha mishipa ya moyo na damu na husaidia kuzuia shambulizi la ugonjwa wa saratani. Kitunguu saumu ni moja ya viungo asilia vinavyotia msukumo zaidi wakati wa uzalishaji wa chembechembe nyeupe za damu.
Hata kwa kuwapo mafanikio ya kisasa za kuondoa matatizio ya vijasumu (antibiotics) na mkanganyiko wa mikrobaolojia, bado kitunguu saumu kinachojulikana na wataalamu wengi wa afya kama tiba muhimu ya maradhi ya maambukizo. Kitunguu saumu hupambana na maradhi tofauti ya utumbo na maradhi mengine ya maambukizo kama vile kuhara damu, homa ya matumbo, mchango uzo na tegu. Kinatoa mafuta ya fushi (fukivu ) yanayochujwa kupitia mapafu na kuyafanya kuwa tiba kabambe ya matatizo ya maambukizo wakati wa kuvuta hewa kama mkamba (bronchi–tis ), ute, mafua na kifaduro.
Mafuta haya vilevile hutumika kutibu kifua kikuu na kusaidia kudhibiti tatizo la pumu. Kitunguu saumu  hupambana na maradhi ya fangasi au ukungu kama ule utoao majimaji ya usaha, mabaka (choa) na kuhusu ukuaji wa bacteria wa manufaa kwa mwili wa binadamu. Pia huweza kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.
Moja ya matumizi maarufu ya kitunguu saumu katika sayansi na teknolojia  yapo katika ugonjwa wa mshituko wa mishipa ya damu ( cardi vascular ) kinaingilia mfumo wa mtawanyo kupunguza viwango vya mafuta katika damu na cholesterol na kupunguza uwezekano wa kuganda kwa damu.
Kwa kawaida, kitunguu saumu hupunguza kasi ya shinikizo la damu na kuzuia utengenezaji wa ziada wa mafuta kwenye mshipa wa damu. Utafiti wa karibuni kabisa umeonesha kwamba kiungo hicho hupunguza ugumu  katika mishipa ya damu inayozeeka.
Allicini ni moja ya viambato vinavyotoa mchango mkubwa katika kuwezesha kitunguu saumu kuzuia uzalishaji wa seli za saratani na kukuza uwezo wa mfumo wa kinga katika kupunguza usambazaji wa uvimbe wenye kudhuru. Pia hutibu vidonda, sikio, majipu, chunjua na kuimarisha  nguvu za uzazi (aphrodisiac)
Watanzania tutumie vitunguu saumu japo vina harufu inayochukiza  kwa kuimarisha afya zetu.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

No comments:

Post a Comment