Pages

Tuesday, December 17, 2013

ARTEMISIA ARFA KIBOKO YA MALARIA



Familia; Compositae
Jamii za porini za Artemisia hustawi katika hali ya hewa ya joto dunia nzima. Artemisia arfa ni ya asili na imekuwa ikitumiwa miaka mingi iliyopita na watu kwa kutibu homa na magonjwa mengine. Huko nchini China na Vietnam wanatumia Artemisia annua ya mbegu mbili tofauti iliyotokana na mimea ya asili ya huko ya Artemisia. Na Artemisia annua ndiyo inayotumika kutengeneza dawa mseto ya malaria hapa Tanzania. Artemisia arfa inastawi katika maeneo ya tropiki, hutoa majani kwa wingi, na majani haya yana Arteminisin kwa wingi, kitu ambacho kinafaa sana kutibu malaria, mmea huu hukua hadi kufikia urefu wa mita 3 lakini haustahimili theluji. Hapa nchini Tanzania Artemisia arfa huota porini. Kwa kuzingatia faida ya mmea huu umefika wakati kwa watanzania kuanza kuotesha katika bustani zetu ili usije ukapotea.
Mmea wa Artemisia arfa pamoja na kutibu malaria pia hutibu magonjwa kemkem  yakiwamo kuvimba kwa utumbo mkubwa (colitis), Ukimwi kwa  kuwa waathirika wa ukimwi wana upungufu wa kinga ya cellular na kinga ya humoral iliyo juu, vichomi, huleta hamu ya kula, utando mweupe mdomoni (candida), majipu, kichocho, kikohozi, mafua, sinusitis, magonjwa ya macho na conjunctivitis, macho mekundu, homa ya matumbo(Typhoid) ikichanganywa na mmea wa Cape Gooseberry. Watu wa mwambao wa pwani (Tanga) hutumia mmea huu kwa kuuchoma kama ubani kwa kuondoa mapepo mabaya (mashetani) huuita kwa jina la pakanga. Pia hutumika kutengeneza juisi kwa maji baridi yaliyo salama kwa kuchanganya na malimao na sukari. Kinywaji hiki ni mbadala mzuri wa soda ya dukani ukizingatia faida zake.
Hutumika kutengeneza dawa ya magonjwa ya ngozi kwa kuchanganya na mafuta ya mbogamboga. Hutumika kuhifadhia nafaka ili zisiharibiwe na wadudu. Ni dawa ya kuzuia magugu yasiote kwa kusambaza majani kwenye ardhi. Wizara ya afya na ustawi wa jamii kitengo cha utafiti wa tiba asilia kifanye utafiti wa mmea huu kwa kushirikiana na waganga wa tiba asili na mbadala.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

3 comments: