Pages

Wednesday, August 30, 2017

LEONOTIS NEPETIFOLIA MMEA UNAO TIBU KIHEREHERE CHA MOYO NA MAPIGO YASIYO YA KAWAIDA



Nilipokuwa kwenye shughuli zangu za utafiti wa mimea 4/6/2017. Niliona mimea aina ya LEONOTIS NEPETIFOLIA maua yake yakiwa yamezungukwa na nyuki wengi sana wakitafuta chakula. Nyuki hao ndiyo walionifanya niandike makala fupi ya mmea huu.
Leonotis Nepetifolia una majina mengine kama Annual lion’s ear, lion’s ear, klip dagga, gran tiparani, Flor de mundo, mota, Christmas candlestick, shandilay, na bradi-bita. Mmea huu hukua kutoka mita moja mpaka tatu. Mbegu zake husambazwa na maji, matope sehemu yauamopita magari na wanyama.
Leonotis Nepetifolia una alkaloids (leonurine na stachydrene), Iridoid glycoside (Leonuride), Iridoid glycosides (leonurin and leonuridine) diterpenoids (leocardin), flavonoids (rutin, quercetin, hyperoside, apigenin), volatile oil, tannins na vitamin A.
Mmea huu maua yake hupendwa sana na wachunga ng’ombe na vijana huko vijijini wananyonya maji matamu yaliyomo ndani ya maua yaani nectar.
Majani hutibu matatizo ya tumbo, kuuma tumbo, arthritic, kisukari aina ya-2 diabetes mellitus, kizuia pumu, kuzuia kuharisha, homa, malaria, kikohozi, womb prolapsed, kutuliza kiherehere cha moyo, hufanya moyo uwe na nguvu katika utendaji wa kazi, tachycardia, mapigo yasiyo ya kawaida ya moyo (irregular heart beats), kuongeza utokaji wa mkojo, uvimbe, thrush, plasta kwenye vidonda na kaswende. Mchemko wa majani na ukanywewa hutibu kuwasha na magonjwa ya ngozi.
Mizizi hutibu matatizo ya Tumbo. Kwa wale wanaoshughulika na mambo ya nyuki na Asali mmea huu unafaa sana kuwa chanzo cha kupata Asali nzuri.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


No comments:

Post a Comment