Pages

Thursday, August 11, 2022

MBAAZI HUTIBU HOMA YA MANJANO


 

Ni mmea wenye jamii ya mikunde. Mbaazi ni zao lenye matumizi mengi na huvumilia ukame. Matumizi muhimu zaidi yanatokana na mbegu zake ambazo zinatumika kuanzia zikiwa mbichi na baada ya kukauka. Jina la kibotania huitwa Cajanus Cajan. Wanyakyusa huita IMBANGE, wagogo huita Mhanje na Wakaguru huita Mhange. Waingereza huita Pigeon pea. Matumizi mengine ya mmea wa mbaazi ni shina lake linalotumiwa kama kuni, majani yanatumika kama dawa na chakula cha mifugo na mizizi yake ni dawa na hurutubisha ardhi. Mbaazi hulimwa katika nchi nyingi za kitropiki kama Tanzania, Kenya, Malawi, Uganda na Nigeria. Mbaazi ni chanzo kizuri cha vitamin B, chuma, na Calcium nk.  Majani hutibu kikohozi, kuharisha, maumivu ya tumbo, vidonda vinavyotoa usaha (sores), Surua, maumivu ya njia ya mkojo, homa ya manjano, upungufu wa damu, hepatitis, kisukari na muwasho wa ngozi sehemu za utupu za mwanamke. Maua yakichemshwa hutibu Mkamba (Bronchitis), Nimonia (pneumonia), kikohozi cha kawaida, kuhara damu na matatizo ya hedhi.  Mizizi hutibu kikohozi (cha kawaida) chimba mizizi ya mbaazi vipande vitano. Chemsha katika maji kiasi cha nusu lita mpaka ibakie kikombe kimoja. Iache ipoe, matumizi mgonjwa mtu mzima anywe nusu kikombe mara tatu kwa siku. Mtoto anywe kijiko kimoja kikubwa mara tatu kwa siku. Itumiwe kwa siku 3.

Ukitafuna mizizi hutibu maumivu ya meno. Mizizi pia hutibu magonjwa ya zinaa  ikichanganywa na mizizi ya ndulele. Mbaazi mbichi na kavu hutumika kwa mapishi mbali mbali ni mmea unaofaa sana kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

 


Mazingira Natural Products

Mbeya

Simu; +255 754 807401, +255 719 564276

Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

Blogu: mazingiranp.blogspot.com

No comments:

Post a Comment