Pages

Thursday, August 11, 2022

WAFUGAJI WA KUKU CHANGAMKIENI MIMEA HII

 Wafugaji wengi wa kuku Tanzania wanafuga kuku kwa mazoea ya kizamani. Leo nimeamua kuwaelezea mimea imayofaa kwa kuku. Lysine inayokuza kuku kwa haraka na kuongeza uzalishaji na methionine inayokuza kuku kwa haraka na kuongeza utagaji wa mayai mengi.
1.    Mmea aina ya Tumbaku ya wazuka (Dandelions) watu wengi hupanda kama maua ya bustani. Lakini kwa binadamu unatibu zaidi ya magonjwa 18. Mmea huu una vitamin A,B,C,E na K. Pia  una madini ya chuma, magnesium, phosphorus, potassium, zinc na calcium. Ukiwalisha kuku mara kwa mara hufanya kiini cha yai kiwe cha njano sana.
2.    Majani ya mchicha nafaka na mbegu zake ni chakula bora sana kwa kuku na mbegu zake zina lysine kwa wingi.
3.    Majani ya Russian comfrey ukiwalisha kuku mara kwa mara kiini cha yai huwa cha njano sana
4.    Mmea wa msemwasemwa (kyusa) (Rumex usambarensis) ukilisha kuku hufanya kiini cha yai kuwa cha njano sana.
5.    Majani ya mlonge (Moringa oleifera) hufanya kiini cha yai kuwa cha njano sana.
6.    Majani ya upupu unaowasha (sting’ing nettle) yana vitamin A,C,D,K na B complex. Yana calcium, magnesium, Chromium, cobalt, chuma, phosphorus, potassium, zinc, shaba na salfa. Ukikausha majani yake kivulini au kwenye kaushio la jua (solar drier) yanafaa sana kwa kulisha kuku kwa kuchanganya kwenye vyakula.

No comments:

Post a Comment