Pages

Tuesday, December 17, 2013

UYOGA CHAKULA KITAMU, FAIDA NA HASARA ZAKE KWA BINADAMU.



Uyoga ni  chakula, tena wanaokifahamu  vizuri  wanakwambia  ni  chakula  kitamu. Mbali ya kuula , Uyoga UYOGA una faida nyingi kwa binadamu. Uyoga  kama  chakula  una tumika  kwa  namna nyingi tofauti naunaliwa  karibu  katika  kira sehemu  duniani. Wakati kwa  AFRIKA, UYOGA unaonekana kwamba nichakula  cha  kawaida ,kwaULAYA na  MASHARIKI MBALI (ASIA) ni chakula muhimu  na cha gharama  kubwa. kwa leo nitaelezea uyoga aina chaza  (OYSTER MUSHROOM) Pleorotus  florida (PFM) – mweupe Pleorotus floridanus(PFST )-Kahawia na wa porini. Uyoga wa Pleorotus  florida (PFM) na Pleorotus  Floridanus (PFST) ndio unaolimwa sasa katika mikoa ya mbeya, iringa, Ruvuma,  Morogoro, Rukwa,pwani DSM, Arusha ,Kilimanjaro ,NK. Watanzania naomba tuchangamkie  kilimo cha uyoga.
Kina faida nyingi. wengine wanaula katika saladi, wengine wanatumia kuongeza ladha  katika mayai, nyama, mchuzi wa tambi, wengine wanatengeneza supu na matumizi mengine tofauti.
VIINI LISHE NA FAIDA ZA UYOGA KATIKA KULINDA AFYA YA MWANADAMU.
Siku  hizi watu  wengi zaidi wanakuwa makini sana na vyakula wanavyokula ilikulinda afya zao .Baadhi ya vyakula hususanif  vile vyenye LEHEMU ama mafuta mengi husababisha maradhi mbalimbali mwilini kama shinikizo  la damu na mengineyo. Uyoga unapotumiwa kwa chakula kamwe hauleti madhara  yoyote bali faida nyingi hazipatikani katika vyakula vingi tunavyotumia. Katika uyoga kuna kiasi cha kutosha  cha protini ,kabohaidreti  na nishati. Lehemu (cholesterol) ambayo husababisha shinikizo la damu  na mengineyo ambayo hupatikana katika aina mbalimbali za protini, haipo kabisa katika uyoga.
Kadhalika ni katika protini za uyoga pekee ambako hupatikana aina zote tisa (9) muhimu za amino asidi ambazo ni muhimu katika kila mlo wa binadamu. Milinganisho ya protini, kabohaidreti , na lehemu na nguvu kati ya UYOGA  na aina mbalimbali za nyama ni kama ifuatavyo . ASIDI ambazo ni muhimu katika kila mlo kamili wa mwanadamu .


Virutubisho
Nyama mbichi ya kuku
Nyama mbichi ya ng’ombe
Samaki kibua mbichi
Uyoga
Protini (mg/100g)
20.5
2013
17.4
12.2
Kabohaidreti (mg/100g)
0
0
0
5.1
Lehemu/ mafuta (mg/100g)
69
59
50
0
Nishati/Nguvu (kj/100g)
506
514
518
334

Kadhalika uyoga una aina mbili za vitamini, zikiwemo Thiamine (vitamin b1) riboflavin (vitaminiB2) Ascorbic Acid (vitamin C) Pamoja na folic acid. Utumiaji wa mara kwa mara wa uyoga hutoa ulinzi wa kutosha dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu  wa vitamin mwilini (kama  vile Beriberi,Pellagra Na Scurvy).
Uyoga mkavu una viini lishe vifuatavyo (1) Protini 20% -45% (2) vitamini B,C,D,E,K,        (3) Madini Calcium, Phosphorus, Chuma, na kiasi  kidogo cha mafuta na mengineyo .
TIBA: Husaidia kutibu/ kupunguza shinikizo la damu, kisukari, vidonda vya tumbo, saratani (kansa), Figo, moyo, uvimbe, vidonda vya mwili, kiungulia, vipara, fangasi aina zote, kifua kikuu, kuongeza kinga ya mwili na kuuwezesha kupigana na magonjwa mbalimbali, kuyeyusha na kusaga takataka zenye asili ya kaboni. Huongeza maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha, saratani ya damu (Leukemia), Ini na mengineyo mengi.
Uyoga unafaa sana kwa waathirika wa UKIMWI.
Faida nyingine ya uyoga ni kusafisha mazingira kwa vile uyoga huoteshwa kwa kutumia mabaki yatokayo mashambani, viwandani na nyasi (majani ya maharagwe, mpunga, randa za mbao n.k). Kuotesha uyoga kwa kutumia takataka hizo ambazo zingekuwa kero kwa jamii ni njia mojawapo ya kusafisha mazingira na mabaki yakishatumika kuoteshea uyoga yanafaa sana kurutubisha ardhi (Mbolea).
MADHARA/ HASARA: - Si uyoga wote unaofaa kwa chakula, kwa sababu aina nyingine za uyoga una sumu inayoweza kumdhuru mtumiaji hadi kumletea kifo. Hakikisha unakula uyoga unaokubalika na si kila aina ya uyoga.
Jinsi ya kufanya kilimo cha uyoga au kuotesha wasiliana nami.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com





2 comments:

  1. Hakika ni zao lenye faida kubwa kiafya, kukuza kipato na kutunza mazingira.
    Tangu nimeanza kilimo hiki ni zaidi ya miaka mitatu sasa sijajuta.Tunauza uyoga mkavu na mbichi, mbegu bora,Tunatoa mafunzo na ushauri,uanzishwaji na usimamizi wa miradi ya Uyoga.
    Tunapatikana Dar es Salaam.
    Twitter/Instagram/Facebook: Hertu Farms
    Simu: 0783182632/0713600915
    Whatsup: 0757315931

    ReplyDelete