Pages

Sunday, August 24, 2014

MAAJABU YA CHOROKO ( CICER ARIETINUM L )




Choroko zao muhimu jamii ya mikunde linalolimwa na kutumiwa duniani kote, hasa nchi za kiafrika na kiasia. Waingereza huita chickpea . Ni chanzo kizuri cha wanga na protini, na protini yake inachukuliwa kuwa ni bora kuliko ya mikunde mingine.  Choroko ina kiasi muhimu cha asidi ya amino za msingi kasoro asidi zilizo na salfa “sulphur“ ambazo zinaweza kukamilishwa kwa kuongeza nafaka katika mlo wa kila siku . Kwenye  kuna hifadhi ya wanga , ikifuatiwa na nyuzinyuzi za chakula, oligosaccharides na sukari rahisi kama vile glucose na sucrose. Ingawa kunapatikana kiasi kidogo cha mafuta ( lipids) choroko ina utajiri wa asidi  za mafuta zisizodhuru muhimu kwa virutubisho kama vile linoleic na oleic acids. Kwenye punje za choroko pia kunapatikana madini ya calcium , magnesium , phosphorus, chuma na K.
            Choroko ni chanzo kizuri cha vitamin muhimu kama vile riboflavian ( vit B2), niacin ( vit B3), thiamin ( vit B1), Folate na vitamin A (B-Carotene) kama ilivyo mikunde mingine choroko ina sababu za kuondoa virutubisho visivyofaa ( ant – nutritional factors) kutokana na mbinu mbalimbali za mapishi choroko zina faida kadhaa kiafya na muunganiko wake   na mikunde na nafaka nyingine unaweza kuwa na athari nzuri kwa magonjwa ya binadamu kama vile kisukari aina ya pili ( type 2 diabetes)  magonjwa  ya mmeng’enyo wa chakula, na baadhi ya saratani, kuondoa udhaifu wa mwili, uchovu na mengineyo, homa, magonjwa ya mfumo wa kupumua na kukojoa, abscesses, husaidia upungufu  wa damu mwilini, hurekebisha lehemu ( cholesterol) na mengineyo.
            Kwa wale wenye kusumbuliwa na matatizo ya nguvu za uzazi  na hawana matatizo ya mzunguko wa damu, mfumo wa neva  mfumo wa mkojo, homoni na kemikali na utendaji  wa viungo vingine ni vizuri wakatumia choroko mara kwa mara.  Wananchi wa nchi za Asia kama India , China ,Japan , Indonesia na nyingine zinatumia sana choroko, soya, dengu nk. Nchi hizi zina watu wengi duniani kuliko hata  ukubwa  wa  nchi zao.  Na utumiaji wa choroko mara kwa mara kwa watu wenye kisukari hurekebisha kiwango cha sukari kwenye insulin.  Watanzania wote tuanze kutumia choroko  mara kwa mara ili kuimarisha nguvu za uzazi kwani sasa hivi  vijana wengi wanalalamika kuwa hawana nguvu za uzazi .
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com



No comments:

Post a Comment