Pages

Sunday, August 24, 2014

FAIDA ZA TENDE KATIKA MWILI




Katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, tende ndio tunda linaloliwa kwa wingi,pengine kuliko tunda linguine. Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia lime thibitika kusheheni madini na vitamin lukuki, hivyo kuwa na faida nyingi kiafya. Katika makala hii, nimekuorodheshea faida 10 za tende:
1.      Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hilo.
2.       Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1,B2, B3,B5, A1na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili kwa ujumla.
3.      Ulaji wa tende huimalisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinacho sababisha maumivi wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.
4.      Ukila tende, mwili utapata nguvu na kuondolea uchofu ndani ya nusu saa, kwasababu tende ina virutubisho vya asili kama vile ‘glukosi’ ‘sucrose’na fructose’. Ili kupata faida za tende, changanya na maziwa fresh kasha kula. Pindi unajisikia mchofu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ina shauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kurejesha mwili wako nguvu, iliyopotea siku nzima.
5.      Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishwaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji wa vyakula vinavyotengeneza ‘potassium’ huweza kumwepusha mtu kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza cholesterol mwilini na LDL Cholesterol.
6.      Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), waweza kupata haueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango chakutosha cha madini ya chuma ambayo huitajika utengenezaji wadamu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
7.      Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, loweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kasha asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo kitafunguka na kuwa laini.
8.      Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalumu wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.
Asubuhi, sisage tende kwenye maziwa hayo hadi zichanganyike, kasha weka asali kiasi cha vijiko vitatu ua vine  vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo, Kisha kunywa mchanganyiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.
          9 Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina mana kwamba, wale wanahitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.
10   Tende inatibu saratani ya tumbo. Hata hivyo tende ni tiba kama tiba nyingine na haina madhara  yoyote kwa sababu ni dawa asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za ‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya macho na tatizo la kuona usiku (night blindness).
     Kwa ujumla faida za tende ni nyingi na unaweza kuila  tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizo 10 na nyingine.

No comments:

Post a Comment