Pages

Sunday, August 24, 2014

MAAJABU YA PARACHICHI (AVOCADO-PERSEA AMERICANA MILL)



Wanyakyusa  na wandali  huita takapela au kasokela. Ni mti  wenye urefu  wa hadi meta 20. Asili yake ni  amerika  ya  kusini  katika  nchi  ya Mexico  na  nyingine. Wenyeji wa Mexico  wa Aztec  neno Avocado lenyewe linatokanana na  neno la Nahuatl  ‘ahuacatl’ ni kifupi  cha neno la kia-Aztec ‘ahuacacuahatl’ likimaanisha mti wa kende/korodani (testicle tree). Parachichi lilipelekwa Ulaya na wahispania  walioenda Amerika ya kusini miaka mingi iliyopita. Hapa Tanzania parachichi  lililetwa na wajerumani na  waingereza kwa nyakati tofauti. Hapa nchini ni watu wachache wanaojua faida za mti huu. Tunashukuru kwa hapa Tanzania, Chuo kikuu cha Sokoine, Tengeru na taasisi  ya  utafiti ya kilimo  Uyole  Mbeya zinafundisha  na kuzalisha parachichi zinazokua kwa muda  mfupi kuanzia miaka miwili na nusu na kuendelea kwa njia ya kupandikiza ‘grafting’. Parachichi (Avocado) ni mojawapo ya matunda ambayo yanatunza na kukuza mwili. Yana vitamini nyingi sana, madini na pia mafuta halisi yanayopatikana kwenye vyakula,  yaani yasiyotengenezwa na binadamu parachichi ina madini, nyuzi na vitamini. Parachichi lina ubora wa vitamin C, B6 na E ambazo ni vitamini muhimu sana za kukuza mwili na pia kwa  afya ya ngozi. Vitamini B6, ukosefu wa vitamin hii huleta kufadhaika  yaani  “mood swings”. B6 pia husaidia  kupunguza maumivu yanayoletwa na hedhi  yaani ‘Premenstrual stress’ PMS. Vitamin C ni muhimu  kwa kuponya vidonda vya ngozi pia husaidia mwili kujikinga na magonjwa  kama mafua na ugonjwa  wa  kuvimba ufizi unaotoa damu  yaani ‘scurvy’. Parachichi ni bora kwa watu  walio  katika  hali  ya kupona  baada  yakuugua  na wale wanaougua pia. Vitamini E  hupunguza kuchoka kwa  akili na  kuongeza  tukio la  uzazi (Upungufu  wa nguvu za  kiume). Vitamini  hii pia ni muhimu kwa afya  ya  ngozi. Madini K+ ni muhimu sana  kwa  maisha ya chembechembe  za mwili  ‘Cells’. K+ ni muhimu kwa  afya kwa sababu  upungufu wake huleta ugonjwa wa kujisikia mlegevu  au kupungukiwa na nguvu. Madini ya parachichi  ni muhimu kwa kukuza mtoto aliye bado tumboni  mwamaake. Parachichi pia matukio ya saratani  furani haswa zile za mdomo  na kishimo kilicho nyuma ya pua, kinywa na koromeo (yaani pharynx) na pia ugonjwa wa moyo. Parachichi ina manufaa kwa mzuguko wa damu mwilini. Majani machanga ni dawa ya kikohozi, yakitokoswa kwenye maji  na yaliyokauswa  kijani nyeusi  ni dawa ya kuharisha. Majani huongeza  damu mwilini [anemia], kuumwa kichwa, koo, tumbo, uchovu, kuimarisha meno na kuondoa maumivu. Maganda [barks] yanafaa kwa kutengeneza dawa rheumatism kwa kuchanganya na mafuta ya mboga mboga. Peke la parachichi ni rafiki mkubwa wa moyo  wa binadamu, majipu, kuimarisha kinga ya mwili na shida ya mkojo  kukwama. Parachichi  hutumiwa  vizuri hufanya kazi ya kuokoa nywele  zinazoanguka (upaa) kama litapakwa pale na husaidia kukuza nywele  zinazodumaa (dandruff). Pia hutumika kwenye vipodozi  mbalimbali. Parachichi hutumika kwa kutengenezea  kinywaji cha parachichi. Kupaka kwenye mkate, ndizi, viazi, magimbi, kutengeneza kachumbali ,guacamole, avocado na saradi ya nyanya, na avocado spread.
Tunapenda kila famiilia kutumia parachichi katika mlo ili kuboresha afya zetu.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 


Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com





No comments:

Post a Comment