Pages

Saturday, April 28, 2018

MACHUNGWA HUZUIA KUPATA SARATANI YA TEZI DUME



Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa kwa wingi Tanzania. Machungwa ni zawadi nzuri ya asili toka kwa mwenyezi Mungu. Asili ya machungwa ni china. Kuna aina  za machungwa Navely, mandarin, caracara, blood oranges, valencia na Seville nk.  Jina  la kibotania huitwa Citrus sinensis au citrus aurantium. Waingereza  huita orange na wandali huita uluki. Machungwa yana vitaminim B,C, calcium, thiamin, riboflavin, nia cin, vitamin B6, folate, pantothenic acid, phosphorus, magnesium, manganese, selenium,  na  shaba. Chungwa  moja lina asilimia 130 ya vitamin C kiwango kikubwa kuliko matunda mengine, na ambacho huhitajika kutumika mwilini kila siku, vitamini A asilimia 2, calcium  asilimia 6. Pia machungwa yana choline, zeaxanthin na carotenoids ambavyo ni muhimu kuimarisha misuli ya mwili, kuleta usingizi mzuri, kuimarisha kumbukumbu na kuzuia saratani ya tezi dume. Matumizi ya juisi ya machungwa hukinga na kutibu kiharusi yakichanganywa na Barungi kwa kiharusi kinachowapata wanawake aina ya Ischemic, kupunguza shinikizo la juu la damu, kupunguza saratani ya damu kwa watoto (childhood leukemia), kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa machungwa yana nyuzi nyuzi, potassium, vitamini C, na choline kwa wingi. Wenye kisukari nao pia watumie machungwa pia hukinga/hutibu Beriberi, homa, hasa homa ya matumbo, Tb na Surua dyspepsia, kufunga choo, mifupa na meno, maradhi ya watoto kama upungufu wa damu na matege, Juisi yake ikichanganywa na chumvi kidogo na kijiko kimoja cha asali hufaa kwa wenye TB, pumu, Bronchitis, kikohozi na common colds, matatizo ya kifua, kuungua mishipa ya damu, kusafisha damu, kuimarisha kinga ya mwili kuimarisha nguvu za uzazi kusaga chakula, kuimarisha mirija ya uzazi,  kutuliza kichefuchefu kwa wajawazito, kuimarisha ngozi ya mwili isiwe na mikunjo na figo. Ni vizuri unapotumia juisi ya machungwa weka na Asali. Wenye mafua waongeze maji ya moto katika juisi ya chungwa kisha  wainywe. Maganda yake yakisuguliwa usoni ni dawa ya chunusi zote (pimples & acne). Maua yaliyokaushwa yakisagwa na kutiwa katika maji moto ni dawa ya shinikizo la mishipa ya Fahamu. Kwa pumu, kikohozi, kuumwa kichwa (kipandauso) chemsha kiganja 1 cha majani katika lita  1 ya maji kwa dakika 3 na kunywa siku moja. Pia machungwa hutumika kutengeneza Juisi, Jamu, mamaledi na mvinyo. Pia Ganda linaleta hamu ya chakula na kusaidia kuyeyusha chakula. Katakata ganda chemsha vijiko 10 vya mezani katika lita moja ya maji kwa dakika 3, kamua na kunywa siku nzima.
 pia tunatoa ushauri, mafuta ya waliopooza na Tiba
Mazingira Natural Products
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com


No comments:

Post a Comment