Pages

Saturday, April 28, 2018

MGOMBA MWITU HUTIBU MIFUPA ILIYOVUNJIKA




 Mgomba Mwitu ni jamii ya migomba. Nimelazimika kuandika makala ya mmea huu, nilienda safari wilayani Rungwe niliona nyani wawili wakila ndizi za mmea huu. Nyani hao walinikumbusha mbali wakati wa utoto wangu tukichunga ng’ombe tulikuwa tunakula ndizi zake kutuliza njaa. Miaka hiyo nilikuwa sijui faida ya mmea huo zaidi ya kutuliza njaa na kiu ya maji. Mmea huu hulimwa sana Ethiopia kwa ajili ya chakula. Hapa Tanzania huota porini na wengine hupanda majumbani mwao kama mapambo. Jina la kibotania huitwa Ensete Ventricosum, majina mengine huitwa Ethiopian Banana, Abyssinian banana, na Ensete false banana. Kwa Kiswahili huitwa mgomba mwitu. Wanyakyusa huita Ibangalala, wameru huita mukobo. Ndugu Erick Saimon Ngao alisema wasafwa huita Kogo(makogo). Ndugu Asunta Ndunguru alisema wamatengo huita mahigo. Mmea huu hupatikana Sudani, Ethiopia, West DR Congo, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Tanzania, Angola, Zambia, Malawi, Zimbabwe na Msumbiji.
Majani na shina hutibu Ini, Hepatitis na wanawake ambao mimba zinaharibika mara kwa mara, kurahizisha wanawake kujifungua vizuri wanapokuwa na uchungu, kuunga mifupa iliyovunjika kutokana na ajali.
Matatizo ya Ini na Hepatitis hutibiwa na majivu ya Tunda la mmea huu na majani, pia hutoa mimba zilizoharibika tumboni, utomvu wa tunda lake hutibu tatizo la kimeo kirefu kwa watoto, wamatengo hutumia kumpa maji ya mmea huu na mbatawata mtoto aliyetoka kukatika kitovu ili atoke nje na kuonana na watu wengine. Jimbi (Corm) lake hutumika kuondoa kondo la nyuma kwa ng’ombe. Wengine hupanda kama mapambo nyumbani na wengine hupanda kuzuia radi isilete madhara.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

3 comments:

  1. Habari. Mizizi yake ipoje mgomba mwitu

    ReplyDelete
  2. Habari. Tiba ya mgomba mwitu kwa mifupa iliyovunjika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi huwa asumbuliwa na uti wa mgongo

      Delete