Pages

Saturday, April 28, 2018

MACHAUCHAU HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI



 

Machauchau ni miongoni mwa mimea inayodharaulika na watanzania wengi pengine kwa kutokujua faida zake kwa afya ya binadamu. Hapa Tanzania wanyakyusa na wachaga matunda yake hulisha Ng’ombe, mbuzi na Nguruwe. Wanyakyusa mboga yake huliwa wakati mboga zingine ni adimu.
Asili ya machauchau ni Mexico, Costa Rica na Brazil nk.
Jina la kibotania huitwa Sechium Edule. Waingereza huita chayote.  wachaga huita machauchau. Australia huita choko, Brazil – chuchu, Philipines -  Sayote , Hawaii – pipinola, Jamhuri ya Dominic – Tayota.
Machauchau ni mmea unaotambaa kama pasheni na kuwa na matunda yanayofanana na baadhi ya maboga lakini matunda yake ni madogo kuliko maboga.  Machauchau yana vitamin B1 (Thiamin), B2 (Riboflavin), B3 (Niacin), B5 (Pantothenic acid), B6 (Pyridoxine), B9 (Folate, Folic acid), choline, vitamin E (Alpha – tocopherol), vitamin K (Phylloquinone), vitamini C kwa wingi, calcium, chuma, magnesium, phosphorus, potassium, sodium. Zinki, shaba, manganese na selenium kidogo na Amino Acids
Machauchau hupunguza uzito wa mwili, Huzuia watoto kuzaliwa bila hitilafu, Hupunguza lehemu, Huzuia saratani, Ni chanzo kizuri cha stamina, Huzuia kuzeeka mapema, chanzo kizuri cha Antioxidants, Hutibu mawe ya kwenye figo, huzuia kutopata choo (constipation), Hushusha shinikizo la juu la damu (HBP – high blood pressure), Hutibu gesi tumboni, Huzuia magonjwa ya moyo, Huzuia Anemia, Hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi, Hutunza thyroid kuwa na afya njema, Husaidia kuzuia maumivu ya miguu na kuongeza kinga ya mwili. Watanzania tuanze kuchangamkia mmea huu kwa ajili ya afya zetu.

Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com

No comments:

Post a Comment