Pages

Saturday, September 6, 2014

MAAJABU YA NETTLE (URTICA DIOICA)







Nettle ni majani ya mimea ya upupu. Ni familia ya urticaceae. Wanyakyusa huita indandye na waingereza huita stinging nettle. Nettle ni mmea unaopatikana mashambani na porini wenye manyoya ya kujikinga aina ya vijimwiba. Hupandwa pia katika bustani za miche. Hupandwa pia katika bustani za miche.
Wakulima na wafugaji huwa hawapendi mmea huu kwa sababu ukigusana na ngozi ya mwili huwasha sana. Lakini nafikiri hawaupendi  kwa kutojua faida zake laiti wangejua faida zake wangeheshimu sana.
Ni mmea unaoweza kukua kwa meta moja hadi tano kutegemea mazingira yaliyopo. Sehemu inayotumika ni majani na mizizi. Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia wajerumani walikuwa na upungufu wa pamba katika kutengeneza nguo ndipo walipotumia kamba ya nettle kutengeneza nguo. Pia askari wa roma wakati wa baridi walitumia nettle ili kuleta joto mwilini kwa kile kitendo chake cha kuwasha pale  unapogusa mwili.
Nettle hutibu kusafisha damu, figo, minyoo, kuhara damu, baridi ya bisi, tezi la shingoni (goita), homa ,  kuumwa mgongo, kusafisha njia ya mkojo, kuongeza damu, dawa ya kikohozi, hutibu maumivu , tonic ya nywele, pumu, kutoka damu puani na mdomoni, kuondoa takataka zisizofaa mwilini, kuhara, kutoa makohozi mapafuni, kuondoa mawe ya kwenye kibofu, uterine hemorrhages, kutibu magonjwa ya ngozi, kuondoa mba kichwani na kufanya nywele kuwa imara jongo(gout) HBP( high blood pressure), hay fever, matatizo ya hedhi, kulainisha ngozi  ya mwili, na ni nzuri kwa maradhi yote ya mzio(allergy) nk.

TAHADHARI
Usile majani mabichi yanaweza kuharibu figo. Majani yaliyopikwa ni lishe nzuri na husaidia utokaji wa mkojo. Majani mabichi yavunwe ukiwa umevaa glavu(Gloves), shati la mikono mirefu na suruali kwa maana  yakishikwa yanawasha sana.
Na usiwape watoto chini ya miaka miwili bila ushauri wa daktari.  Na kwa vijana wadogo wa kuanzia miaka 65 na kuendelea waanze dozi na dozi ndogo na kuendelea kuwa kubwa.
Ni vizuri tuanze kulima, kuilinda na kuihifadhi Nettle.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


No comments:

Post a Comment