Pages

Saturday, September 20, 2014

MMEA WA COMFREY(RUSSIAN COMFREY-SYMPHYTUM OFFICINALE AU PEREGRINUM) WENYE MANUFAA KWA SICKLE CELL




Komfrey ni mmea uishio miaka mingi. Ina umuhimu kwa mboga zenye afya kwa familia, pia malisho bora kwa wanyama wengi. Majani ya mmea huu huweza kutengenezwa mbolea kwa ajili ya bustani.
Russian Comfrey-Symphytum Peregrinum au Officinale) ni mmea uliopatikana katika mapori ya milima ya Kaukasus-Urusi. Pengine ndio maana ukapewa jina la Russian Comfrey. Mmea huu ulipelekwa uingereza-ulaya katika karne iliyopita na kutoka Uingereza ulisambazwa Canada, Amerika, Australia, New Zealand na Afrika.
Waingereza ndio walioleta hapa Afrika ya Mashariki. Mmea huu hupandwa zaidi katika mikoa ya Ruvuma,Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa n.k. Mmea huu haufai kupandwa katika nyanda za upepo wenye joto au sehemu zenye joto ukanda wa Pwani. Hii ndiyo sababu Comfrey inaweza kupandwa katika kivuli cha upenu wa nyumba au miti. Na watu wengine hupenda kuuita mboga tumbaku kwa sababu majani yake yanafanana na ya tumbaku.
Comfrey ni mmea ujengao Protini upesi zaidi kuliko mimea mingine iliyopo. Zaidi ya protin una viini muhimu vya vitamin na hasa kiasi cha juu zaidi cha vitamin B12 ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa seli mwilini.
Kwa maana hii mmea huu unafaa sana kutumiwa na wenye matatizo ya Sickle Cell, Sickle Cell hushambulia chembechembe za damu. Pia kwa kiasi ni ugonjwa wa kurithi. Sehemu zenye ugonjwa wa Malaria kwa wingi ndio huathirika zaidi. Unatumia majani, na pia unaweza kuchanganya na mchicha, Chinese, Swiss Chard au mboga za maboga. Mchanganyiko huu ni muhimu sana katika kupambana na matatizo ya Sickle Cell. Unga wa majani uliokaushwa kwa kaushio la jua (Solar driers) ni muhimu kwa kuongeza protini ndani ya vyakula mbalimbali kama supu, mchuzi wa mboga (ugali), uji n.k
Pia majani mabichi au yaliyoanikwa unaweza kutumia kwa chai kwa kuongeza asali/ sukari, utaboresha afya yako kwa kinywaji hiki.
Magonjwa mengine yanayoponywa kwa kutumia Comfrey ni jeraha, michubuko ni uvimbe wa miguu na mikono. Majani na mizizi ndivyo vinavyotumika kutengeneza dawa.
Comfrey  ni malisho muhimu kuwakilisha samaki na wanyama. Ni malisho bora kwa wanyama wenye tumbo moja kama kuku n.k kwa sababu ina nyuzi kidogo zaidi kuliko mimea mingine. Inasaidia kujenga mifupa. Kwa ng’ombe wa maziwa hutoa maziwa mengi. Comfrey kwa mbolea (hupata potashi kufunika udongo kwa majani ya Comfrey (Mulching) hasa kwa nyanya na viazi.
Ni vizuri zile sehemu ambazo unastawi wananchi wakachangamkia na kuupanda ili kupata faida zake.
Ukifanya jitihada za kututembelea ofisini utajua tunatibu maradhi mengine pia ikiwamo homa ya matumbo (Typhoid), Malaria, michirizi inayosababishwa na ujauzito( Stretch Marks in Pregnancy), mkanda wa Jeshi (Herper Zosters), Matatizo ya meno, Magonjwa ya ngozi, tumbo, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa gesi tumboni, kupunguza makali ya saratani, kisukari, BP ya kupanda. Mengine ni pamoja na maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto, vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 

Mazingira Natural Products
Mbeya
Simu; +255 754 807401, +255 719 564276
Barua pepe; mnp.kaka@gmail.com


No comments:

Post a Comment