Pages

Wednesday, April 6, 2016

MCHAICHAI HUFAA KWA MAUMIVU YA HEDHI



Mchaichai hupandwa sehemu nyingi Tanzania. Mchaichai hupandwa sehenu yenye rutuba na tifutifu na kwenye kivuli kidogo.
Gawanya mmea ulio stawi na kupanda.Majani hufikia hadi sm 50 urefu. Mwagilia Maji vizuri katika hatua ya awali. Jina la kibotania huitwa cymbopogon citrates. Waingereza huita lemon grass, barbed wire grass, silky heads, citronella grass, fever grass. Michaichai haihitaji uangalizi wa hali ya juu, na bora ikapandwa katika kila bustani, Zahanati na hospitali. Mchaichai hutibu maumivu makali wakati wa hedhi kwa kuchanganya na pilipili manga, shida ya umeng’enyaji wa chakula tumboni, homa  kwa kushusha joto la mwili, huzuia na kutibu mkazo wa msuli, kutibu ringworm, kutibu baridi yabisi, maumivu ya kiuno Neuralgia, kuteguka unachanganya mafuta ya mchaichai na mafuta ya nazi na kuchua sehemu iliyo athirika. Kama maumivu yanaendelea tumia mafuta ya mchachai tu bila kuchanganya na ya Nazi, vilevile husaidia kwa maumivu ya meno, kipindupindu na tumbo kujaa gesi, pia husaidia kumfanya mtu kukojoa sana , kutapika, kuharisha, nzuri sana kwa ukosefu wa usingizi, Mchaichai ni mzuri kwa kila mwenye tatizo la maumivu mbalimbali, pia unatibu  magonjwa yanayopatikana kwa kutumia  masufuria ya aluminium na shinikizo la damu, Bawasiri kwa kuchanganya na majani ya mwembe au mkaratusi, Malaria na harufu mbaya mdomoni.
Dozi: weka kiganja 1 majani katika maji lita moja 1 yaliochemka, kwa dakika 15: kunywa nusu kikombe kutwa mara tatu (3) kwa siku.
Matatizo ya kifua, mafua na sinusitis- chemsha kiganja kimoja (1) cha mchaichai kwenye lita moja ya maji na vuta mvuke wake.
Sehemu nyingine duniani mchaichai hutumika kama kiungo katika vyakula na kuongeza harufu katika mvinyo.
Mchaichai hutengenezwa mafuta ya watoto na mafuta ya kuchulia, D away a mafuta kwa ajili ya  mwili. Dawa ya mafuta kwa bawasiri, kutengeneza na sabuni na dawa ya kufukuza wadudu na nyoka.   

Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil) na Tiba. 
Mazingira Natural Products
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com

No comments:

Post a Comment