Pages

Wednesday, April 6, 2016

NGENGELE ZAO LILILOSAHAURIKA

Tumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutufikisha mwaka 2016 salama na wale ambao wametangulia mbele za haki mungu awapumzishe salama.
Nimeamua kuandika makala hii baada ya kutoka safarini wilayani RUNGWE. Wakati wa matembezi yangu niliona mmea ninaoufahamu umepandwa kwa mzee mmoja wa kinyakyusa.
Nikakumbuka kuwa hata mimi nimepanda nyumbani kwangu Mbeya. Ikabidi nimwone huyo mzee ili niweze kupata maelezo ya mmea huo na akanikaribisha.
Nikajitambulisha mimi ni nani na natoka wapi. Na yeye akajitambulisha yeye ni nani. Ndipo nilipomweleza shida yangu iliyonipeleka kwake. Yule mzee aliniambia kuwa ule mmea ameurithi kutoka Kwa baba yake mzazi. Akanieleza kuwa miaka zaidi ya 50 njaa iliwahi kutokea unyakyusani na viazi hivyo viliwaokoa wakati wa njaa. Na akaniambia kwamba mzee wake alisema kamwe asiupoteze maishani mwake. Mmea huu kwa kibotania huitwa Dioscorea bulbifera. Waingereza huita Air potato au Bitter yam, Wanyakyusa huita ngengele. Na husitawi kwa mtindo wa kutambaa kwenye miti kama chayote au pesheni.
Na inaweza kukua inchi 8 kwa siku na wastani kufikia futi 60.Na huweza kufika futi 150 kwa urefu kufuatana na eneo lilivyo rafiki na mmea wenyewe. kuna aina zingine ni chungu na haziliwi. Dioscorea bulbifera na Dioscorea Deltoidea ndio huliwa. Lengo langu kubwa ni kwa watanzania kuanza kufufua mazao yaliyokuwa yakilimwa na mababu zetu na kutumiwa kwa chakula lakini yameachwa kwa sababu ya kwenda na wakati.
Huko Kenya kabila la Tiriki wanaita marugu (Dioscorea bulbifera) wanasema ni chakula bora kuliko mkate wa ngano mweupe.Wanasema wakila marugu hukaa muda mrefu tumboni bila kusikia njaa. Hapa Tanzania tunatakiwa tuendeleze zao hili na yale mengine ambayo hayatiliwi maanani.
Dioscorea bulbifera ina flavonoids na isoflavonoids vitu ambavyo ni muhimu kwa afya zetu.
Ngengele huzuia/ hutibu kuharisha, kuhara damu, Homa ya manjano, maumivu ya tumbo, Anorexia, conjunctivitis, na mzio unaosababishwa na kuumwa na wadudu kama spider na whip spider. Wenzetu wahindi na wachina hutumia kutibu maumivu ya koo, saratani ya tumbo na goita. Wapangwa wa Ludewa huita Ing’ing’i hutumia kuondoa matego kwa watu waliofanyiwa hivyo. Wanyakyusa hula baada ya kuvichemsha au kuviweka kwenye majivu ya moto mpaka vikaiva. Aina ya Dioscorea deltoidea huliwa na wale wanaotaka kuwa mabaunsa (body-builders) na wale wanaotaka kuongeza Testosterone mwilini.
                                          ANGALIZO
Kuna aina nyingi za Ngengele zingine ni chungu unapokula, kwa hiyo hakikisha unatumia zile ambazo zinafaa kuliwa. Ngengele haziko kundi moja na viazi vitamu.

No comments:

Post a Comment