Pages

Wednesday, April 6, 2016

MAHARAGE YA KIJANI HUPUNGUZA LEHEMU NA KISUKARI



Maharage mmea huu unapatikana karibu kila sehemu duniani,Kuna aina tofauti zaidi ya 500.Leo nitaelezea aina ya maharage ya kijani Haricot vert maana ya maneno haya hutokana na lugha ya kifaransa.Haricot maana yake maharage na vert ni kijani. Maharage haya huchumwa yakiwa machanga na kuliwa pamoja na maganda yake.Maharage haya pamoja na mengine ya kawaida kama kidney beans, Navy beans na black beans nk. Kwa jina la kibotania huitwa phaseolus vulgaris. Waingereza huita Beans (string beans) katika nchi nyingine ni mbegu tu zinazoliwa.Lakini maharage mabichi na maganda yake pia ni chakula chenye thamani. Kwenye maharage ya kijani kuna vitamin A, C, E, K, vit. B1, B2, B6, nyuzinyuzi, calcium, potassium, phosphorus, protini,shaba, magnesium, choline,niacin, chuma,folic acid,omega 3fatty acid, chromium na silicon nk.
Maharage ya kijani ni dawa ya kuongeza mkojo,hufanya moyo kuwa na afya njema kutokana na kuwa na vitamin A na C  kwa wingi, kuimarisha mifupa na hata wale waliovunjika kwa kuwa yana vitamin K kwa wingi inayoshughulika na kuimarisha mifupa, maharage ya kijani hufaa kwa wenye kisukari aina ya 2 kwa kuwa yana nyuzinyuzi nyingi zinazofaa kwa wenye kisukari kuendelea kuishi maisha ya kawaida, hufanya Colon kuwa na afya njema, wanaosumbuliwa na Arthritis na pumu wawe wanakula mara kwa mara watapata nafuu, Eczema, wanaotaka kupunguza uzito wale mara kwa mara haya maharage, wanawake waja wazito wale mara kwa mara kwa kuwa yana folic acid ya kutosha, hupunguza lehemu mwilini, hupunguza uwezekano wa kupata kansa ya matiti, hupunguza matatizo yanayotokana na kukoma kwa hedhi kwa wanawake,Jongo (Gout), maumivu ya kuvimba kwa viungo (baridi  yabisi) na magonjwa ya figo nk. Kwa wale watakaotumia maharage yaliyo kwenye maganda yaliyokaushwa gramu 10 hulowekwa katika lita 1 ya maji usiku kucha, halafu yanachemshwa baadaye yanachujwa. Kunywa wakati  wa mchana kwa wagojwa wenye kisukari tiba hii hupunguza kidogo kiwango cha sukari katika damu.
 Pia tunatoa ushauri, mafuta kwa waliopooza na wanobabuka na jua kama Albino (Herbal sunscreen oil)
na Tiba.                                              
Mazingira Natural Products
Mbeya.
Simu: +225 754 807401-0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu: mazingiranp.blogspot.com

No comments:

Post a Comment