Pages

Friday, May 18, 2018

KOMAMANGA HUSAIDIA KUONDOA SUMU MWILINI



Komamanga ni moja ya matunda yenye faida kwa afya ya binadamu. Komamanga limekuwa likilimwa kwa miaka zaidi ya 5000 iliyopita huko mashariki ya kati. Komamanga linakua hadi kufikia kimo cha Meta 5 -10 kutegemea eneo. Jina la kibotania huitwa Punica granatum linn. Waingereza  huita Pomegranate. Hulimwa sana nchini India. Pia hili ni tunda linalopatikana sana Afrika Mashariki. Tunda la komamanga lina protini, nyuzinyuzi, wanga, calcium magnesium, oxalic acid , phosphorus, chuma, sodium,potassium, shaba, sulphur, chlorine, Vitamin A, vitamin B1, B5, Vitamin E, riboflavin, Nicotinic acid na vitamin C. komamanga  ni chanzo kizuri cha sukari, (glucose na Fructose), vitamin C na chuma,. Pia komamanga lina utajiri mkubwa wa kuleta nguvu mwilini. Juisi ya komamanga lililoiva ni nzuri kwa Homa ya matumbo, Gastric na Homa za pumu. Juisi ya komamanga ni nzuri kwa wenye high blood pressure kwani inapunguza hali hiyo. Juisi ya komamanga ikichanganywa na Asali ni nzuri kwa wenye umri mkubwa  kwa ajili ya kuimarisha kumbu kumbu iliyopotea. Upungufu  wa damu changanya juisi ya tunda la komamanga kikombe kimoja cha chai, ¼  tsp mdalasini na Asali 3tsp na kunywa. Pumu na kikohozi changanya juisi ya komamanga, Tangawizi mbichi na Asali kwa kiwango sawa. Tumia kijiko cha chakula mara mbili kwa siku. Mbegu za tunda changanya pilipilimanga na chumvi kidogo mpatie mgonjwa wa homa ya manjano. Juisi ya komamanga na ndimu pamoja ikitumiwa mara tatu kwa siku ni nzuri kwa matatizo ya Ini na homa ya manjano. Komamanga hutibu matatizo ya njia ya mkojo , Juisi ya ya tunda hilo husaidia kuponya saratani, husaidia mtiririko wa damu kwenda vizuri kwenye mishipa. Hali hiyo husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, na kiharusi, ulaji wa mara kwa mara wa tunda hilo huzuia meno kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu na maambukizi ya virusi ndani ya mwili, husaidia pia kutibu maradhi ya tumbo ikiwamo kutopata haja kubwa, komamanga husaidia kuondoa sumu mwilini, kupambana na tatizo la uzito, komamanga hutibu magonjwa ya muda mrefu kama saratani ya tezi dume, saratani mbalimbali, kisukari, baridi yabisi na jongo (gout), kuweka sawa mfumo wa chakula na njia ya usagaji wa chakula. Mbegu za komamanga, magome na mizizi yakichemshwa na maji ni  dawa ya minyoo aina tapeworms. Gome na ganda la ndani la komamanga (Rind) ni dawa ya kuwasha ngozi na koo. Pia hutumika kuosha utupu wa mwanamke unaowasha na kuweka vizuri cervic. Juisi ya komamanga ni nzuri  kwa wenye umri mkubwa kwa Figo na kibofu cha mkojo kuwa na nguvu za kufanya kazi vizuri. Kuharisha damu: tumia juisi ya majani mabichi machanga. Maganda ni tiba ya kuharisha na kuhara damu. Majani na maua hutibu virusi vya macho (conjuctivities virus). Magome hutibu bandama, vidonda vya koo, homa na leucorrhea yakichemshwa. Saga mbegu na weka ndani ya maziwa hutibu mawe katika figo. Dozi ya magome, majani au maua tumia gramu 10 hadi 15 katika lita ya maji. Pia tunatoa ushauri, mafuta ya waliopooza na tiba zingine.

Mazingira Natural Product
Simu: +255754807401/- 0719 564 276
Barua pepe:mnp.kaka@gmail.com
Blogu:mazingiranp.blogspot.com

No comments:

Post a Comment